Na Mwandishi wetu, TimesMajira,Online
WANANCHI wa Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha wakiongozwa na viongozi pamoja na Mbunge wao wameunda kamati ya
takribanI watu 60 yenye lenjo la kuratibu mapendekezo ya wananchi kuhusu mgogoro wa ardhi katika tarafa ya Ngorongoro pamoja na Mgogoro wa kilometa za mraba 1500 uliopo Tarafa ya
Loliondo na Sale.
Akizungumza jana wilaya humo mkoani Arusha, Mwenyekiti wa viongozi wa Kimla Ngorongoro, Metui Oleshaduo wakati akisoma tamko la kamati hiyo ya mapendekezo juu ya jitihada za kumaliza mgogoro huo wa ardhi.
Oleshaduo amesema kamati hiyo ya Wilaya inajumuisha wawakilishi upande wa Madiwani, wenyeviti, wawakilishi wa kinamama, viongozi wa kimila na baadhi ya wasomi wa jamii ya kimasai.
Amesema kazi kubwa ya kamati hiyo ni pamoja na kuelekea kutatua migogoro hiyo bila kuathiri pande zote
mbili zinazovutana.
“Kamati hii imeanza kazi ya kukusanya maoni ya wananchi kwa vijiji vyote vinavyozunguka eneo lenye mgogoro wa kilometa za mraba 1500 pamoja na vijjji vyote vya Tarafa ya Ngorongoro ambapo
Mchakato huu utakusanya maoni kwa wananchi,” amesema na kuongeza
Oleshaduo amesema baada ya kuona mchakato wa kuwashirikisha wananchi na makundi ya jamii kuwa hafifu katika kutatua migogoro hiyo, wameona ni muda muafaka sasa kujitafutia njia ambayo mapendekezo yao kama jamii yanaweza fikia wahusika na umma wa Watanzania kwa ujumla.
Amesema kamati hiyo inaendelea kuratibu na kuchakata maoni ya wananchi ili kuandaa taarifa moja ya wilaya inayojumuisha mapendekezo kuhusu mgogoro wa Hifadhi ya Mamlaka ya Ngorongoro pamoja na mgogoro wa Loliondo wa kilometa za Mraba 1500.
Hata hivyo amempongeza Rais Samia Suluh Hassan kwa kumbadilisha waziri wa Maliasili na Utalii na kumshauri waziri wa Maliasili na Utalii Pindi Chana aanze na suaala la Ngorongoro kwa kuzuia propaganda zozote dhidi ya wananchi wa Ngorongoro
hasa Jamii ya Kimasai.
“Pia tunampongeza mwa Rais Samia kumtaka waziri maliasili na utalii asitishe michakato yote inayoendelea na kutoa nafasi ya kusikiliza jamii, tatu kukataza matisho na kamatakamata yoyote dhidi ya wanajamii, viongozi na
watetezi wa haki za binadamu wanaosimama kutetea haki za jamii, kuzuia vitisho dhidi ya
waandishi wanaotoa taarifa za umma, tatu kuzuia Wanangorongoro kuitwa si Watanzania,” amesema
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa