Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma.
MKURUGENZI Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB)Godfred Mbanyi amesema wanafunzi 65 kati ya 427 waliofanya mtihani wa 23 wa kitaaluma ya ununuzi na ugavi wamefeli kabisa ambapo ni sawa na asilimia 14.4% hivyo wanatakiwa kurudia mitihani hiyo katika ngazi ambazo walirisiti kufanya mitihani hiyo huku akielezea kuwa kila ngazi inakuwa na mitihani minne hivyo hao waliofeli wanapaswa kurudia mitihani yote.
Pia amewataka wanafunzi wote waliofeli mitihani na wale wanaotakiwa kurudia kuhakikisha wanajisajili tena kwa ajili ya kufanya mitini hiyo.
Akitangaza matokeo ya mtihani wa 23 ya kitaaluma ya ununuzi na ugavi jijini hapa leo Mbanyi amesema kuwa jumla ya Wadahiliwa walikuwa 479,kati yao waliofanikiwa kufanya mitihani ni 427 ambapo 28 kati yao hawakufanya kabisa mtihani huo huku watahiniwa 230 kati ya waliofanya mtihani wanatakiwa kurudia baadhi ya mitihani waliyofeli (Suplimentary) ili kukidhi ufaulu katika masomo waliyofeli.
“Katika mitihani mingi ya Bodi inayohusisha maswala ya mahesabu ,takwimu, Uchumi na masomo mengine yenye kuhusisha hesabu wanafunzi wamekuwa wakifanya vibaya pia mitihani ya kitaaluma ya Ununuzi na Ugavi kuna wanafunzi pia wamefeli hivyo wanapaswa kufanyia kazi kwa sababu ndio maeneo ambayo watakwenda kufanyia kazi,”amesema.
Ametaja jumla ya Masomo kuwa ni 32 huku akisema kati ya hayo Masomo 6 wamefanya vibaya sana ,17 ni ufaulu wa Wastani na masomo 11 wamefanya vizuri kiasi na kufanya jumla ya wastani wa ufaulu katika mitihani hiyo ya Bodi ya kitaalamu ya Ununuzi na Ugavi kuwa ni asilimia 34.6% kwa mtihani huo wa 23.
Hata hivyo amesema kuanzia Machi 14 mwaka huu dirisha la usajili litakuwa wazi kwa ajili ya wanafunzi watakaohitaji kufanya mitihani hiyo ya bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi ambapo fomu za kujiunga zitapatikana katika tovuti ya bodi hivyo usajili wote utafanyika mtandaoni (Online) na kuwataka wanafunzi kujitokeza kwa wingi kuomba nafasi hiyo ya kufanya mitihani ya Kitaaluma ya ununuzi na ugavi.
More Stories
Kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Ubelgiji lafanyika Dar
CCM kuhitimisha kampeni kwa kishindo
Walimu elimu ya lazima watatakiwa kuwa wabobezi kwenye masomo wanayofundisha