Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema uwepo wa sekta ya kibenki iliyo imara nchini huchangia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la ajira na kutoa fursa kwa wananchi kujiongezea kipato.
Rais Samia amesema hayo katika Hafla ya Uzinduzi wa Makao Makuu ya Benki ya CRDB iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
Rais Samia amesema benki ya CRDB imefanya vizuri katika kutoa fursa za ajira, biashara na ujasiriamali kwa sekta binafsi wakiwemo bodaboda, mama lishe na wamachinga.
Aidha, Rais Samia ameitaka benki hiyo kuendelea kuyawezesha makundi hayo ili kutayarisha walipa kodi na kutanua wigo wa Serikali kukusanya mapato kupitia makundi hayo.
Rais Samia pia amesema Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi za kifedha hukuakiongeza kuwa sekta za kibenki zina jukumu la kufufua uchumi uliodororakutokana na UVIKO 19.
Serikali kupitia Benki Kuu imeanzisha mpango mahsusi wa kuiwezesha sekta ya kibenki kupata mikopo yenye riba nafuu ambapo imetenga jumla ya shilingi Trilioni moja kwa ajili ya kuyakopesha mabenki kwa masharti nafuu zitakazowezesha kuikopesha sekta binafsi nchini.
More Stories
Mwalimu adaiwa kumfanyia ukatili mwanafunziÂ
NAOT watakiwa kuendana na viwango vya ukaguzi
Rais Samia kuzindua mfuko wa kuendeleza kazi za wabunifu