Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya.
SERIKALI kupitia Wizara ya maji imesaini mkataba na Kampuni ya Lahmeyer Consulting Engineers Co.Ltd ya jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusimamia utekelezwaji wa mradi wa Maji wa Mto Kiwira kwa gharama ya shilingi bilioni 2.216 bila kodi ya ongezeko la thamani.
Hafla ya utiaji saini huo umefanyika katika ofisi ya Mamlaka ya Maji na usafi wa Mazingira Mbeya baina ya Mkurungenzi wa Kampuni hiyo Mhandisi Ngwisa Mpembe na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji, CPA Gilbert Kayange na kushuhudiwa naNaibu Waziri wa Maji Mhandisi MaryPrisca Mahundi na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera.
Akitoa taarifa ya Mradi huo, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Mbeya, CPA. Gilbert Kayange alisema mradi huo unatarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia Julai mwaka huu hadi Juni 2024.
Amesema kukamilika kwa mradi huo kutazalisha lita milioni 131 kwa siku na hivyo kumaliza kabisa tatizo la maji katika eneo la Huduma ndani na nje ya Jiji la Mbeya kwa zaidi ya miaka 20 ijayo.
Amesema majukumu ya Mkandarasi mshauri ni kufanya maptio ya usanifu wa mradi, kuandaa vitabu vya zabuni na kuongoza mchakato wa kumpata mkandarasi wa ujenzi  ambayo itakuwa awamu ya kwanza inayotarajiwa kufanyika ndani ya miezi 6 hivyo kukamilika Agosti mwaka huu.
Amesema awamu ya pili itakuwa ni kusimamia ujenzi wa Mradi na kukabidhi mradi kwa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mbeya kwa kipindi cha miezi 24 kuanzia Agosti mwaka huu hadi Julai 2024.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi MaryPrisca Mahundi alimtaka Mkandarasi Mshauri kufanya kazi yake kwa weledi kwa kutafuta Mkandarasi mwenye sifa na vigezi bila kuwa na upendeleo wa undugu na urafiki ambapo Serikali ipo tayari kulipa kila hatua inayohitajika.
Hata hivyo Mhandisi Mahundi alisema kuwa Rais Samia amekuwa akiibua ndoto ya maji kwa vitendo katika kuwaletea wananchi wake maendeleo hivyo ni vema mkandarasi mshauri aliyepewa mradi huo kufanya kazi kwa weledi mkubwa .
“Rais Wetu Mama Samia Suluhu Hassan amekuwa akijitahidi kuhakikisha kuwa wananchi wote wanapata maji safi na salama hivyo ndugu yangu mkarandarasi ulipewa dhamana hii tunaomba usituangushe katika hili “amesema Naibu Waziri wa Maji mhandisi Mahundi.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Dkt.Vicent Anney amesema Mradi huo uwanufaishe Wananchi watakaopitiwa kwa kupewa kipaumbele cha kazi ambazo hazihitaji utalaam pamoja na kupewa maji ili wasaidie kuulinda.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera ameipongeza liipongeza Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia suluhu Hassan kwa kutoa fedha za kuwezesha mradi huo mkubwa kufanyika Mbeya na kumaliza tatizo la maji kipindi cha masika.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi