Muonekano wa ujenzi wa barabara ya Njambe-Ndonga yenye urefu wa kilometa saba inayojengwa kwa gharama ya sh. milioni 69 ikijumuisha na ujenzi wa mitalo, daraja na makaravati, ujenzi huo unaofanywa na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) wilayani Nyasa Mkoa wa Ruvuma. Kijiji hicho kitafikiwa na barabara hiyo kwa mara ya kwanza tangu Uhuru. Mhandisi wa TARURA Wilaya ya Nyasa, Thomas Kitusi akizungumza na waandishi wa habari (hawap0 pichani) juu ya ujenzi wa mradi wa barabara ya Njambe- Ndonga yenye urefu wa kilometa saba ambayo ilikuwa haijawai kuchongwa tangu Uhuru. Mhandisi Thomas Kitusi akielekeza namna barabara ya Njambe-Ndonga itakavyojengwa kwa kupigwa zege maeneo korofi ili iweze kupitika wakati wote wa msimu wa mvua na kiangazi, barabara hiyo hadi kukamilika itakuwa imegharimu kiasi cha sh. milioni 69 fedha za mfuko wa maendeleo. Moja ya barabara ya rami iliyotengenezwa na TARURA wilayani Nyasa kwa fedha za maendeleo kutoka mfuko wa jimbo ambazo zilitolewa na Rais Samia Hassan Suluu kiasi cha sh. Milioni 500. RARURA Wilaya ya Nyasa wameweza kujenga barabara ya rami yenye urefu wa kilometa 1.5 chini ya mkandarasi Ovans. Picha zote na Cresensia Kapinga. Post Views: 828 Continue Reading Previous Dkt.Mpango awafariji wafiwa wa ndugu watano wa familia moja atoa maagizo mazito kwa IGP,vyombo vya ulinzi na usalama mkoa na wilaya ya BahiNext Muheza yapitisha bajeti ya Bilioni 41. 24 katika mwaka wa fedha 2022/23 More Stories Habari Muhoji Sekondari kumaliza changamoto ya umbali kwa wanafunzi Musoma vijijini January 5, 2025 zena chitwanga Habari Tanzania mwenyeji mkutano wa nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika January 5, 2025 Penina Malundo Habari TANESCO yarudisha shukrani kwa jamii January 5, 2025 Penina Malundo
More Stories
Muhoji Sekondari kumaliza changamoto ya umbali kwa wanafunzi Musoma vijijini
Tanzania mwenyeji mkutano wa nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika
TANESCO yarudisha shukrani kwa jamii