Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
- Ataka Ongezeko la uandikishaji watoto Elimu ya Awali na Darasa la kwanza
-Asisitiza kutokana na uhaba wa Ardhi msimamo wa Mkoa ni kujenga Madarasa ya magorofa
- Akemea Uvamizi wa maeneo ya shule, awataka walimu Wakuu kuwasilisha taarifa za migogoro ya Ardhi katika maeneo yao
- Asema Ujenzi wa Madarasa umekamilika Walimu kwa umoja wao waunge Mkono Juhudi na ubunifu wa Rais Samia
- Awataka Walimu kushiriki kikamilifu katika Kampeni mbalimbali zinazofanyika katika Mkoa wa DSM.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla ametoa maelekezo hayo leo Januari 11,2022 wakati wa kikao kazi na walimu wa Kuu wa shule za msingi na Sekondari DSM katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Shaban Robert, Ilala Jijini Dar es Salaam.
Aidha RC Makalla amepongeza kazi inayofanywa na walimu wote wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mkoa umekuwa ukifanya vizuri Kitaaluma kupitia matokeo ya mitihani ya taifa lakini pia hata nyanja za michezo Mkoa umekuwa ukifanya vizuri.
Hata hivyo RC Makalla amesema takwimu za Uandikishaji hadi sasa Elimu Awali ni asilimia 39 na Darasa la kwanza ni asilimia 68 kwa hiyo kasi zaidi inahitajika ili watoto wote wennye sifa waandikishwe.
RC Makalla amekemea michango mbalimbali isiyofuata taratibu ambayo ni kikwazo kwa wanafunzi wakati wa kujiandikisha ambapo amesisitiza watoto wasiziiliwe kwa sababu ya sweta, au mchango wowote.
Vilevile RC Makalla amesema msimamo wa Mkoa kwa sasa ni kutumia vizuri Ardhi kwa kujenga Madarasa ya magorofa kwa kuwa idadi ya wanafunzi imekuwa ikiongezeka kila siku wakati Ardhi ni ilele.
Sambamba na hilo Mkuu wa Mkoa amekemea Uvamizi wa maeneo ya shule na kuwataka Wakuu wa Shule kwa kushirikiana na Watendaji wa Kata na Mitaa kuwasilisha taarifa za migogoro ya Ardhi ili iweze kufanyiwa Kazi, na ameelekeza Wakurugenzi kupima maeneo ya shule.
RC Makalla amesema Ujenzi wa Madarasa umekamilika amewapongeza Walimu wakuu kwa kusimamia vizuri Ujenzi huo tena kwa Kipindi kifupi ambapo Mkoa wa Dar es Salaam umefanikiwa kujenga Madarasa 743 na bweni moja Walimu wana kila sababu ya Kuunga mkono ubunifu na Uzalendo wa Rais Samia Suluhu wa kutafsiri vema matumizi ya Mkopo wa Uviko 19.
Pia RC Makalla amewataka Walimu kushiriki kikamilifu katika Kampeni mbalimbali zinazofanyika katika Mkoa wa Dar es Salaam ikiwemo Kampeni ya SAFISHA PENDEZESHA DSM kwa kuhakikisha maeneo ya shule yanakuwa safi Vilevile Kampeni ya Kuwapanga vizuri wamachinga wahakikishe wanalinda maeneo ya shule yasivamiwe na wafanyabiashara wadogo.
Kwa Upande wa Afisa Elimu Mkoa Ndg Abdul Maulid akitoa takwimu ya Uandikishaji wa watoto Elimu Awali na Darasa la kwanza amesema kwa sasa takwimu zimeongezeka wiki iliyopita Uandikishaji Elimu Awali ulikuwa asilimia 32 na Darasa la kwanza asilimia 52 lakini hadi sasa takwimu zimeongezeka, Elimu Awali asilimia 39 na Darasa la kwanza asilimia 68
More Stories
Rais Samia aungwe mkono ajenda ya nishati safi ya kupikia
Ushiriki wa Samia G20 wainufaisha Tanzania
Dkt.Tulia ashiriki ibada, asisitiza waumini kushiriki uchaguzi serikali za mitaa