Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Jumuhiya ya wanataaluma wa kiislamu Tanzania ( TAMPRO) imefanya mkutano wa mwaka jijini Dar es Salaam na kubainisha mambo matano wanayotarajia kuyafanya katika miaka minne ya uongozi wao ambayo yatakuwa ni dira ya maendeleo kwa kipindi hicho.
Akizungumza na Waandishi wa habari, Mwenyekiti wa TAMPRO, Haji Mrisho amesema mambo yanayotarajiwa kufanyika katika kipindi hicho ni kufanya tafiti Ili kuleta masuluhisho ya changamoto mbalimbali ambazo zinaikabili jamii.
Pia amesema watatoa ushauri wa kitaalamu, kujenga uwezo kwa kupitia mafunzo na kufanya kushawishi na utetezi kwa maana ya kwamba kufanya utetezi katika njia ya kitaalamu hasa kuepusha mambo ambayo yanaweza yakaleta migogoro katika jamii.
Mwenyekiti huyo Aliongeza kuwa katika mikakati hiyo pia wanatarajia kuanzisha Miradi uchumi.
Mbali na yako mwenyekiti huyo amesema mambo ambayo wataendelea kudumu nayo ambayo walikua wakiyafanya ni kujenga ushirikiano na mahusiano na Taasisi na wadau wa maendeleo ikiwemo serikali.
Pia mwenyekiti wa TAMPRO alitoa wito kwa wataalamu wote kufanya kazi kwa weledi na kuleta masuluhisho ya changamoto mbalimbali ambazo zinaikabili jamii;
“Wito kwa wataalamu kufanya kazi kwa weledi iwe kazi ya mfano ili watu waweze kujifunza na awe wakala wa mabadiliko kuleta masuluhisho ya matatizo ya wananchi ambayo wanayo”
Naye Makamu Mwenyekiti wa TAMPRO Dkt. Abubakari Kijoji amesema wanajivunia kwa kuanzishwa kwa saccos ya kwanza ambayo mpaka sasa imeweza kutoa mikopo isiyokuwa na riba yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 10 lakini pia kuhamasisha kuhakikisha kwamba wanaisaidia serikali katika kutoa huduma za kitaaluma.
Dkt. Kijoji amesema Wamekua wakishirikiana na Taasisi nyingi za kitaaluma kwa kutoa utetezi na kushiriki kwa kuchangia chuo kikuu Cha kiislamu.
Jumuhiya ya wanataaluma wa kiislamu Tanzania (TAMPRO) ilianzishwa mwaka 1997 na hadi sasa kina wanachama zaidi ya 200 katika fani mbalimbali ikiwemo Sheria, Uchumi, Uhasimu, Wahandisi, Wataalamu wa masuala ya dini n.k
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa