November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watakiwa kusherehekea siku Kuu ya Krismas huku wakichukua tahadhari ya UVIKO 19

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

WAUMINI wa madhehebu mbalimbali ya kikristo na jamii kwa ujumla wameaswa kusherehekea siku kuu ya Krismasi na mwaka mpya huku wakichukua tahadhari ya UVIKO 19 kwa kuepuka misongamano isiyo ya lazima.

Akitoa ujumbe wa siku kuu ya Krismas ,Mchungaji wa Kanisa la EAGT Ipagala Askofu Dkt.Evance Chande amesema,kirusi kipya ya UVIKO 19 kipo hivyo watu wanapaswa kuchukua tahadhari zote pamoja na kuwalinda watoto kuepuka maambukizi ya kirusi hicho kipya.

“Tuchukue tahadhari ya UVIKO 19 ,kirusi kipya kipo ,tusherehekee sikukuu hizi tukiwalinda watoto ,kutembea na sehemu zenye utulivu na siyo kwa kufanya maovu ,kwenda baa na uzinifu.”amesema Asokofu Chande

Akizungumza kuhusu Siku Kuu ya Krisimas Askofu Chande amesema,siku hiyo ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo ambalo ni muhimu lililosherehekewa zaidi ya miaka 2000 iliyiopita na bado linasherehekewa mpaka sasa.

Hata hivyo amewaasa waumini wa dini ya Kikristo kutosherehekea tarehe ya kuzaliwa kwa Yesu bali kuona umuhimu wa kuja kwake nay ale aliyoyatenda duniani.

“Hata hapa duiani wapo watu maarufu na waasisi wa Taifa letu ambao hatupo nao sasa,lakini tunapowakumbuka hatuhitaji sana tarehe za kuzaliwa kwao bali tunawakumbuka na kuwaenzi kwa kazi walizozifanya katika Taifa letu.”amesema Askofu Dkt.Evance na kuongeza kuwa

“Kwa hiyo ujio wa Yesu ni pamoja na kuleta amani kwa wanadamu ambayo ndio kila kitu na inatakiwa ianze kwenye familia ,jamii inayokuzunguka na Taifa kwa ujumla,

“Hapa nchini tunashukuru tunepata viongoiz wacha Mungu ambao wamefanya watu wake waishi na kuabudu kwa amani .”

Kwa upande wake Mchungaji Dkt.Barnabas Chihekwe amesema,wakati jamii ikisherehekea siku Kuu hiyo Krismasi waumini wa Kikristo watumie imani yao kujenga jamii moja na siyo kutengana wala kudharauliana na dini nyingine

“Tumeitwa kuishi kama jamii yenye mchanganyiko wa imani ,dini na kitazamo mbalimbali lakini tumeitwa kama jamii,wakristo tutumie imani yetu kujenga jamii moja siyo kutengana wala kudharauliana bali kuwa msingi mmoja ili tusonge mbele licha ya kuwa na imani na mitazamo tofauti lakini bado lengo letu ni moja.”amesema Dkt Chihekwe