Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla na Wafanyabiashara wa Soko dogo la Kariakoo wamekubaliana kupisha Ujenzi wa Soko jipya na ukarabati wa Soko lililoungua ambapo wameomba Ujenzi ukikamilika kipaombele Cha kwanza kitolewe kwao.
Akizungumza wakati wa kikao Cha pamoja na Wafanyabiashara hao, RC Makalla amesema taratibu za Ujenzi zinaanza rasmi kesho Disemba 24 Baada ya kukamilika kwa taratibu zote ikiwemo Mkandarasi kupatikana na kusaini mkataba wa Ujenzi.
Aidha RC Makalla amewahakikishia kuwa Ujenzi ukikamilika kipaombele Cha kwanza kitatolewa kwa wale waliopisha Ujenzi.
Ili kuhakikisha waliokuwepo ndio wanapewa kipaombele, RC Makalla amesema kabla hawajaondoka timu itapita kuwaratibu kwa kuchukuwa taarifa zao ikiwemo majina yao na Aina ya Biashara wayayofanya ili pawepo na kumbukumbu.
Hata hivyo RC Makalla amesema wakati wote wa Ujenzi Wafanyabiashara waliokuwepo watahamishiwa masoko ya kisutu na Machinga Complex.
Ujenzi wa Soko jipya la Kariakoo la Gorofa 6 na Ukarabati wa Soko lililoungua unagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 26 ambazo zilitolewa na Rais Samia Suluhu Hassan ili kuweka mazingira Bora ya Wafanyabiashara Kariakoo.
More Stories
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja