Na Tiganya Vincent,timesmajira,online
MKUU wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani amesema wakati wa ujenzi wa bomba ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania ni vema utoaji wa kazi zisizohitaji ujuzi ukakazingatia wakazi wa maeneo ambapo mradi huo unapita ili kuwaimarisha kiuchumi na ulinzi .
Balozi Dkt. Batilda ametoa kauli hiyo leo mjini Tabora wakati akifungua mafunzo ya siku moja ya kuwaelimisha wajumbe wa Kamati ya Usalama na Wakuu wa Taasisi za Umma umuhimu mradi huo kwa maendeleo ya Mkoa na Nchi kwa ujumla.
“ Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anasisisitiza ‘Local Content’ kwenye utekelezaji wa ujenzi wa miradi mbalimbali katika maeneo inapofanyika…Ni lazima tuzingatie hilo wakati tukianza ujenzi wa mradi huo ili vijana wetu wapatie ajira na mamalishe wa Mkoa wangu watoe huduma ya chakula” amesema.
Balozi Dkt. Batilda amesema kazi zote ambazo haziitaji utaalamu kipaumbele wapewe wakazi wa Mkoa wa Tabora na hasa wa Wilaya ya Nzega na Igunga.
Wakati huo huo Balozi Dkt. Batilda amewataka wakazi wa Mkoa wa Tabora kuchangamkia fursa ya ujenzi wa mradi huo kwa kufuga kuku, kulima mazao kwa wingi na kujenga nyumba kwa ajili ya shughuli za biashara.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora amesema kwa upande wa Serikali imeshaweka msingi katika suala la ulinzi kwa kuanzisha ulinzi shirikishi ili kuweka mazingira salama ya vifaa vitakavyotumika katika ujenzi wa mradi huo.
Kwa Upande wake Afisa Mazingira Mwandamizi kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) TPDC Anne Maria Simon ameshauri Chuo wa Ufundi Stadi (VETA) kuangalia uwezekano wa kuandaa kozi ambazo zitawajenga vijana wa Tabora ili waweze kushiriki kwa wingi katik autekelezaji wake.
More Stories
Balozi Nchimbi kuongoza waombolezaji mazishi ya Kibiti leo
Dkt.Tulia,apewa tano kuwezesha wananchi
Nkasi yajipanga kukusanya mapato