January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

St. Mary’s Tabata yaahidi makubwa kitaaluma

Na Mwandishi Wetu,TimesMajira,Online,Dar

SHULE ya St. Mary’s Tabata jijini Dar es Salaam, imeahidi kufanya vizuri kitaaluma kwenye matokeo ya darasa la saba katika mitihani inayotarajiwa kufanyika wiki ijayo.

Hayo yamesemwa hivi karibuni na Mkuu wa Shule ya St Marys Tabata, Thomas Samson , wakati wa mahafali ya 21 ya shule hiyo yaliyofanyika kwenye viwanja vya shule hiyo, Tabata Dar es Salaam.

Mkurugenzi mwenza wa shule za St. Mary’s Hamphrey Rwakatare akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa darasa la saba wa shule ya St Mary’s Tabata jijini Dar es Salaam wakati wa mahafali ya 21 ya shule hiyo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki.

Amesema walimu wamefanyakazi kubwa ya kuwandaa wanafunzi vizuri hivyo hawana shaka kuhusu ufaulu mzuri watakaoupata kwenye matokeo hayo.

“Ndugu wazazi naomba niwahakikishie kuwa tumewaandaa vijana hawa kwa uhakika na wote watafaulu vizuri na kwa kuwa tumeshaanza kusajili wanafunzi wa shule ya awali ni vyema mkawaleta wengine,” alisema

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya St Mary’s Tabata wakionyesha vyeti vyao wakati wa mahafali ya 21 ya shule hiyo yaliyofanyika shuleni hapo mwishoni mwa wiki

Mwalimu Samson amesema shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri kiwilaya na kimkoa katika matokeo ya kitaifa hivyo aliwasihi wazazi waendelee kuwaamini kwa kuwapeleka watoto wao shuleni hapo.

“Kwenye mtihani wa darasa la saba mwaka jana wanafunzi wetu wote walipata ufaulu mkubwa wa wastani wa daraja A jambo ambalo linatufanye tuwe na imani kwamba mwaka huu pia tutafanya vizuri,” amesema

Baadhi ya wahitimu wa darasa la saba wa shule ya St Mary’s Tabata wakiingia kwa mbwembwe kwenye mahafali ya shule hiyo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki.

Akizungumza kwenye mahafali hayo, mmoja wa wakurugenzi wa shule hizo za St Mary’s Humphrey Rwakatare aliwashukuru wazazi kwa kuendelea kuiamini shule hiyo na kuwapeleka watoto wao.

Amesema shule hiyo haitawaangusha kwani imeweka mipango kabambe kuboresha huduma za shule hiyo kuanzia usafiri, chakula na miundombinu mingine ili izidi kupaa kitaaluma.

Mmoja wa wahitimu wa darasa la saba wa shule ya St Mary’s ya Tabata jijini Dar es Salaam, akionyesha mtindo wa mavazi wakati wa mahafali ya 21 ya shule hiyo.

“Tumekuwa tukifanya vizuri kitaaluma mwaka hadi mwaka na tunawaahidi kuendelea kufanya vizuri kitaaluma kwenye mitihani yote ya kitaifa tunaomba tuendelee kushirikiana na mtuletee watoto wenu,” amesema