Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa anatarajia kuzindua programu ya kukuza ujuzi kwa vijana nchini awamu ya tatu baada ya serikali kupitia ofisi ya waziri Mkuu kudhamini vijana 14,440 kupitia vyuo 72 katika mikoa 26 ya Tanzania bara.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama amesema jana Julai 31 mwaka huu wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa mafunzo ya uanagenzi awamu ya tatu yatakayofanyika kitaifa katika Chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia (must) na Mgeni rasmi ni Waziri Mkuu.
Mhagama amesema kuwa uzinduzi huo utafanyika Agosti 2 mwaka huu na kwamba Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu imeelekeza nguvu katika Ofisi ya Waziri Mkuu kwa lengo la kuimarisha utekelezaji wa programu ya kukuza ujuzi nchini kwa kuhakikisha inawafikia vijana wengi zaidi katika mikoa yote nchini ili kuzalisha wataalam katika nyanja mbalimbali serikalini
Akifafanua zaidi Mhagama amesema kuwa mafunzo hayo yanahusisha vijana kutumia asilimia 40 ya muda wao katika masomo ya nadharia huku asilimia 60 ikitumika katika masomo ya vitendo kama sehemu ya kazi.
“Ndugu waandishi wa habari mafunzo haya ya miezi sita yaliyoanza kutolewa mwezi Juni mwaka huu yanatarajiwa kukamilika mwezi Desemba 2021” amesema Waziri Mhagama.
Hata hivyo Waziri Mhagama ameeleza kwamba tangu kuanzishwa kwa programu ya kukuza ujuzi kwa vijana mafunzo hayo yamefanyika kwa awamu mbili ambapo jumla ya vijana 28,941 wamenufaika na kwamba awamu ya tatu imehusisha vijana 14,440.
Amesema kuwa Mkoa wa Mbeya una jumla ya vijana 1,722 ambao wanapata mafunzo hayo kati ya vijana 14,440 wanaopata mafunzo nchini kwa kibali cha Rais Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema kuwa kitendo cha Ofisi ya Waziri Mkuu kuleta mafunzo hayo kuzinduliwa kitaifa mkoani Mbeya ni jambo la msingi Sana
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi