Na Mwandishi Wetu,TimesMajira,Online,Dar
SAMPULI za samaki waliokufa waliokuwa wakielea katika ufukwe uliopo karibu na Hospitali za AghaKhan na Ocean Road jijini Dar es Salaam zimepelekwa kwenye maabara kwa ajili ya uchunguzi.
Sampuli wa samaji hao zimepelekwa kwenye maabara ya TAFIRI, maabara ya Taifa ya Uvuvi (Dar es Salaam) na Polisi Kitengo cha Sayansi ya Uchunguzi (Forensic Investigation) kwa ajili ya kupeleka maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali..
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Wizara ya Mifungo na Uvuvi leo imeeleza kwamba samaki wengine walikabidhiwa kwa Afisa Uvuvi wa Halmashauri ya Jijila Dar es Salaam kwa ajili ya kuteketezwa.
Tukio la kuteketezwa samaki hao lilishuhudiwa na maofisa wa wizara,uongozi wa Soko la Feri, ofisi ya uvuvi Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na wananchi waliokuwepo eneo la Soko la Magogoni Feri.
“Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi inapenda kuwashukuru wananchi wote waliokuwepo kwenye ufukwe wa hospitali za AghaKhan na Ocean Road pamoja na Soko la Magogoni Feri wakati wa tukio hili kwa ushirikiano mkubwa waliouonesha uliofanikisha kuzuia kuingizwa kwa samaki hao sokoni na hatimaye kuteketezwa na afisa uvuvi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam,” imeeleza taarifa hiyo.
More Stories
Kanisa la Shincheonji la Yesu nchini Ufaransa lakanusha ripoti ya Le Parisie
Vyombo vya ulinzi na usalama Mbeya,Benki kuu kushirikiana kutatua changamoto za utapeli mtandaoni
Polisi Mbeya kuimarisha ulinzi kuelekea sikukuu ya Pasaka