January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TABWA waiomba Serikali kuwashika mkono

Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online

JUMUIYA ya Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TABWA),

wameiomba Serikali ya awamu ya sita kuwashika mkono

ili kuwekewa maeneo maalumu ya kuzalishia bidhaa zao.

Akizungumza katika Maonyesho ya 45 ya Biashara ya

Kimatafa (DITF) yanayoendelea katika Viwanja vya

Mwalimu Julias Nyerere Jijini Dar es salaam,

Mkurungezi Mtendaji wa TABWA, Moreen Mawalla amesema

chagamoto kubwa wanayokutana nayo ni kutokuwa na

maeneo rasmi ya kuzalisha bidhaa.

Amesema, mazingira ya utegenezaji wa bidhaa mpaka

kumfikia mraji yamekuwa ni kikwazo kutokana na

kutokukidi vigezo vinavyotakiwa, hivyo wakipata maeneo

Maalumu itasaidia kutegeneza bidhaa za viwango vya juu

“Tunaiomba Serikali yetu iliyopo chini ya Rais Samia

kusikia kilio chetu kwa kutujengea maeneo rasmi kwa

ajili ya kuzalisha bidhaa, jambo hili litamsaidia

mwanamke kutegeneza bidhaa bora zenye viwango na

hatimaye kupata masoko ndani na nje,” amesema Mawalla.

Mawalla amesema, serikali ya awamu ya sita ni sikivu

hivyo wanaimani ombi lao litapokelewa kwani tayari

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan

Suluhu ametilia mkazo kuhusu masuala ya kiuchumi

wanawake.

Hata hivyo, Mawalla amesema wanawake wajitokeza

kushiriki Maonyeshoya hayo na kutaja baadhi ya mikoa

kuwa ni Dar es Salaam, Iringa,Mbeya,Arusha,

Morogoro,Kilimanjaro,Kagera,Dodoma,Pwani na Zanzibar.

Vilevile amesema, mbali na hao pia TABWA imepokea

wafanyabiashara kutoka nchi ya Burundi ambao wamekuja

na vitu mbalimbali .

Naye mmoja wa wafanyabiashara kutoka Burundi

Ndihokuvwayo Jackson amesema, hii ni mara ya saba

kushiriki maonyesho hayo.