November 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Florence Masuka (wa kwanza kulia) Mwenyekiti Jumuiya ya wazazi Mkoa wa Dar es Salaam akipata maelezo katika Banda la STAMICO kwenye Maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

UWT Dar watembelea banda ya STAMICO Sabasaba

Na David John,TimesMajira Online, Dar

VIONGOZI wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania(UWT) kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Dar es Salaam wametembelea mabanda mbalimbali kwenye Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere Wilayani Temeke.

Miongoni mwa mabanda yaliyotembelewa na viongozi hao wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam akiwemo Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Tifa ya  CCM(NEC) Angel Akilimali ni banda la Shirika la Madini la Taifa(STAMICO).

Wakiwa hapo maofisa na watalaam wa STAMICO wa kada mbalimbali walitumia nafasi hiyo kuwaeleza viongozi hao wa UWT shughuli wanazozifanya huku wakionesha wakiwaonesha sampuli za makaa ya mawe ambayo yanatumika kutengeneza mkaa mbadala ambayo yalionekana kuwavutia viongozi hao na kutaka kujua faida zake na jinsi yanavyotumika.

Akifafanua zaidi, sababu za kuamua kutembelea banda hilo la STAMICO, Akilimali amesema pamoja na mambo mengine shirika hilo limekuwa likiendeleza wachimbaji wadogo wa madini na kuwajengea uwezo wa kuchimba madini katika mazingira yasiyo hatarishi kiafya.

“Tunawashuku STAMICO kwa kupata fursa ya kutembelea hapa pamoja na mabanda mengine yaliyomo humu, tumekutana na wajasiriamali wanawake , tumejifunza na kupata uzoefu wao katika shughuli wanazofanya zikiwemo katika sekta ya madini.

“Lakini kwenye sekta ya madini akina mama wengi walikuwa bado waoga wanaogopa, walikuwa hawana muamko, hivyo kwa kutembelea kwetu tukitoka hapa tunakwenda kuhamasisha wanawake wa UWT ili waweze kukimbilia fursa hiyo.

“Wanawake wasiogope kwani wanaweza, na kama katika mabanda hayo ya madini kuna wanawake ambao wameweza basi na wanawake wengine wanaweza, hivyo ni kuchangamkia fursa kwa kujitokeza kufanya shughuli za uchimbaji madini,”amesema

cha muhimu ni kupata tu uelewa na kujengewa uelewa na kupata mtaji ili nao waweze kuthubutu kuingia katika sekta ya madini.