November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Songwe kushirikiana na TMDA kuwaongezea uwezo wakaguzi wa dawa

Na Esther Macha,TimesMajira Online, Songwe

MGANGA Mkuu wa Mkoa wa Songwe,Dkt.Nyembea Hamad amesema kuwa wanashikiriana na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA)katika kuwaongezea uwezo wakaguzi wa dawa na bidhaa afya kwa katika vituo vya kutolea huduma za afya ,maabara pamoja na maduka yanayouza bidhaa Afya katika Mkoa huo .

Mganga Mkuu mkoa wa Songwe Dkt.Nyembea Hamad

Amesema kuwa wameweka msisitizo mkubwa katika eneeo kwasababu kumekuwa na changamoto ya Mkoa huo kuwa mpakani kumekuwa na bidhaa ambazo zimekuwa zikiingia kwa njia ya panya ambazo hazijasiliwa na zipo kwenye soko hivyo kutokana na hiyo wamekuwa wakishirikiana na TMDA kuwawezesha wakaguzi kubaini bidhaa ambazo hazijasiliwa na zipo sokoni na bidhaa zilizoisha muda wake na feki.

Dkt. Nyembea amesema hayo jana wilayani hapa wakati akifungua mafunzo kwa wakaguzi wa dawa ngazi ya halmashauri ambapo alisema matumizi ya dawa bila kufuata taratibu za watalaam zimekuwa zikileta usugu wa vimelea dhidi ya dawa ambazo zimekuwa zikitumika kutibu magonjwa ambayo yamesabishwa na vimelea .

Hata hivyo Mganga Mkuu huyo amesema matumizi ya dawa bila kuandikiwa na wataalam zimekuwa zikileta madhara ,baadhi ya dawa zinaandikwa hospitalini lakini mteja akitumia haponi ambapo inapekelea sababu mbali mbali ikiwemo kuingia kwenye soko kinyemela na zinakuwa haziko sawa na zingine na dawa zingine zimekuwa zikitumiwa na watu zilizoisha muda wake .

Amebainisha kuwa hali hiyo imekuwa ikitokea sababu ya ukaguzi hafifu au wakaguzi ambao hawana uwezo mkubwa .

Aidha Dkt.Nyembea amesema kuwa anaamini kuwa tatizo hilo litakwisha baada ya kufanya kazi vizuri baada ya kujengewa uwezo watafanya usimamizi mzuri kwenye vituo na maduka mbali mbali kuweza kuhakikisa kuwa huduma zinazotolewa zinakuwa bora na dawa sahihi pamoja na vifaa vya maabara vitenganishi vinafanya kazi vizuri ili kuweza kutoa majibu yaliyo sawa na mteja kupewa dawa iliyo sahihi.

Kwa upande wake Meneja wa Kanda wa mamlaka ya dawa na vifaa tiba (TMDA)Anitha Mshighati amesema kuwa lengo la mafunzo kwa wakaguzi wa dawa ni kuwajengea uwezo wakaguzi waliopo katika halmashauri ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi .

Hata hivyo Meneja huyo amewataka wakaguzi kutumia kihalali madaraka walinayo na si kwa manufaa binafsi na kwamba awali baadhi ya wakaguzi walikuwa wakitumia vibaya vitambulisho vilivyopita .