LONDON, England
MASHABIKI takribani 60,000 wanatarajia kushuhudia mashidano ya Kombe la Mataifa Ulaya Euro 2020, hatua ya Nusu fainali na fainali itakayofanyika kwenye Uwaja wa Wembley, England baada ya kufantika mazungumzo kati ya serikali ya Uingereza na UEFA.
Hapo awali, ripoti zilionyesha kwamba Budapest inaweza kuchukua nafasi ya Wembley kama uwanja utakaotumika kwa hatua hizo wakati wa wasiwasi ulipotanda vizuizi vya coronavirus vitaendelezwa huko England, huku Italia ilipendekeza jiji lake la Roma.
Hata hivyo, makubaliano yamefikiwa kati ya serikali ya Uingereza na UEFA kuongeza idadi ya wahudhuriaji huko Wembley hadi uwezo wa asilimia 75.
Rais wa UEFA, Aleksander Ceferin alisema, anamshukuru Waziri Mkuu na serikali ya Uingereza kwa bidii yao katika kukamilisha mipango hiyo na wao, ili kufanikisha mashindano hayo hatua ya mwisho huko Wembley.
Nusu fainali na fainali zitachezwa Julai 6, 7 na Julai 11 kutashuhudiwa umati mkubwa zaidi uliokusanyika kwenye hafla ya michezo nchini Uingereza kwa zaidi ya miezi 15.
More Stories
Samia awazawadi Stars milioni 700/-
Samia atoa bilioni 8/- kukarabati viwanja vya CHAN, AFCON
Rasmi Chatsoko mdhamini mkuu wa Goba Hills Marathon 2025