Na Grace Gurisha, TimesMajira Online
RAIS wa zamani wa klabu ya Simba, Evans Aveva na makamu wake, Godfrey Nyange maarufu Kaburu wanatarajiwa kuanza kujitetea Juni 29, 2021 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kupatikana na kesi ya kujibu.
Mbali na washtakiwa hao mshtakiwa mwingine katika keshi hiyo ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hansppope.
Kesi hiyo leo ilikuja mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kwa ajili ya kuanza kusikilizwa kwa upande wa utetezi, baada ya washtakiwa hao kukutwa na kesi ya kujibu.
Wakili wa Serikali, Silvia Mintato amedai, wakili anayeendesha kesi hiyo, amepata udhuru wa safari kwenda Dodoma, na kuomba kupangiwa tarehe fupi kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa na Hakimu Simba alikubaliana na ombi hilo kisha kuahirisha kesi hiyo hadi Juni 29, 2021 kwa ajili ya washtakiwa kuanza kujitetea.
Awali, Mahakama hiyo ilitupilia mbali pingamizi la upande wa Jamhuri la kupinga dhamana ya Aveva na Kaburu hadi pale rufaa yao waliyokata Mahakama Kuu ya kupinga kuondolewa shtaka la kutakatisha fedha dhidi ya washtakiwa hao litakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
Hakimu Simba aliwaachia Aveva na Kaburu kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili waliosaini bondi ya Sh. milioni 30 kila mmoja na kuwa na vitambulisho vya Taifa.
More Stories
Watumishi wa Fahari wafanya Bonanza
Rais Samia atia mkono mchezo wa masumbwi Tanzania
Chino bingwa mpya wa IBA Intercontinental Championship