January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ukanda wa Gaza washambuliwa

GAZA, Serikali ya Israel imefanya mashambulizi ya anga katika Ukanda wa Gaza baada ya wanamgambo wa Kipalestina kurusha maputo yenye vilipuzi Kusini mwa Israel.

Hali hiyo imetokea yakiwa ni makabiliano ya kwanza kati ya pande hizo mbili tangu kuzuka mzozo mkubwa mwezi Mei, mwaka huu ambapo mamia ya watu waliuawa.

Mashambulizi hayo ni ya kwanza chini ya serikali mpya ya muungano inayoongozwa na Waziri Mkuu, Naftali Bennett, aliyechukua nafasi hiyo Jumapili baada ya kuondolewa kwa waziri mkuu wa zamani, Benjamin Netanyahu.