Na Mwandishi Wetu, TimesMajira online, Arusha
MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imetakiwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kubaini uwepo wa dawa bandia na pia kuhakikisha bidhaa zilizopo sokoni ni salama na zenye ubora.
Hayo yamebainishwa leo na Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Arusha Vones Uiso kwenye mkutano wa kikao kazi na wahariri ulioandaliwa na TMDA mkoani Arusha.
Amesema kuwa ili TMDA ifikie malengo inatakiwa kuhakiki usalama na ubora bidhaa hizo sokoni kabla ya kumfikia mwananchi ili kuepuka madhara yatokanayo na matumizi ya dawa bandia.
Hata hivyo amevipongeza vyombo vya habari ambavyo vimekuwa vikitoa taarifa mbalimbali hususan umuhimu wa udhibiti bidhaa kwani imesaidia kuongeza uelewa kwa jamii.
Ameviomba vyombo vya habari kushirikiana katika utoaji wa taarifa za uwepo wa dawa bandia mbalimbali ambazo ni hatari kwa afya za wananchi.
“TMDA haiwezi kutekeleza majukumu yake bila ushirikiano wa vyombo vya habari hivyo ni vyema mkawaelimisha wananchi hususan wafanyabiashara kuacha mara moja kununua dawa,vifaa tiba na vitenganishai kutoka maeneo yasiyo rasmi na meneo ambayo ni kinyume na sheria kwani mara zote bidhaa hizo huwa si salama kwa matumizi ya walaji
“Ikumbukwe kuwa Serikali haitamuonea huruma yeyote atakayebainika kuwa na bidhaa duni ama bandia kwa kigezo kuwa hawakujua wakati huo huo na kusababisha madhara,’ amesema Uiso.
Amesema kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Samia Salumu katika jitihada za kuboresha utoaji huduma miaka ya 1990 ilianzisha progamu ya kuboresha utoaji huduma katika sekta ya uuma ili kufikia matarajio ya jamii.
Uiso amesema kuwa mojawapo ya mikakati katika progamu hiyo ni kuanzishwa kwa wakala mbalimbali Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba na TMDA ikiwa ni mojawapo.
“Wote ni mashahidi wa umuhimu wa taasisi hii hususani katika kipindi hiki cha majanga ya dunia, mlipuko wa magonjwa kama vile Corona na magonjwa mengine.
“Tofauti ya dawa, vifaa tiba ni bidhaa nyeti zinazoweza kuwa na madhara makubwa za kiafya kwa watumiaji kama vile kusababisha ulemavu kupoteza maisha na kudhoofisha uchumi wa nchi kama hazikudhibitiwa ipasavyo,” amesema.
Amesema kuwa bidhaa hizo zinahitaji kudhibitiwa kwa utaratibu na namna ya pekee ili kuzuia madhara ya namna hiyo kwa walaji.
Pia ina jukumu la kudhibiti matangazo ya bidhaa za dawa, vifaa tiba na vitenganishi ili kuzuia matangazo yenye nia ya kupoteza umma kwa lengo la kibiashara ambapo sheria yake ilianza kutumika tangu 2010.
Naye Mkurugenzi Mkuu TMDA,Adam Fimbo amesema kuwa itakapofika Julai mwaka huu TMDA itakuwa imefikisha miaka 2 tangu 2019.
Katika utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu ch Dar es Salaam Desemba 2020 kuhusu namna ambavyo wateja wanavyorishwa na huduma imebainika kuwa katika Halmashauri 28 na mikoa 14 ya Tanzania wamebaini kuwa asilimia 47 tu ya wananchi ndio wanaifahamu TMDA.
“Ni dhahiri kuwa kwa matokeo hayo ni ni kwa sababu ya mabadiliko yaliyofanyika hivyo kupitia vyombo vya habari vyombo vya habari vitaongeza hiyo asilimia na kupanda zaidi na kufahamika zaidi nchini,’ amesema Fimbo.
Fimbo amesema kuwa upo umuhimu mkubwa wa jamii kuifahamu TMDA na sheria inayosimamiwa na kwa utaratibu huu hivyo kupitia kikao kazi hiyo anaamini kuwa kwa ushirikiano wa karibunu kila mmoja ataweza kufahamu majukumu yao kupitia vyombo vya habari.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa kikao kazi hicho kitafanyika kwa siku mbili ambapo malengo yake ni matano ikiwamo ni pamoja na kuelimisha waandishi juu ya sheria zilizopo , majukumu na kazi za TMDA, mchango wa vyombo vya habari katika kulinda afya ya jamii, kufuata sheria na kununi zilizozowekwa na kuendeleza ushirikiano ili kurahisisha kazi ya udhibiti wa bidhaa.
More Stories
NAOT watakiwa kuendana na viwango vya ukaguzi
Rais Samia kuzindua mfuko wa kuendeleza kazi za wabunifu
Makalla ampongeza Lissu kukiri CHADEMA haina wagombea Serikali za Mitaa