Na Zena Mohamed,TimesMajira Online-Dodoma
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira,Seleman Jafo ameongoza matembezi ya hiari ya upandaji miti ikiwa na lengo la kukijanisha Dodoma kuelekea Siku ya Mazingira Duniani.
Matembezi hayo yamefanyika leo jijini hapa kutoka viwanja vya Bunge kuelekea eneo la Medeli ambapo shughuli ya upandaji miti imefanyika.
“Lazima tulinde nchi yetu maeneo mengi leo hii yamegeuka kuwa jangwa,mji huu ulikuwa hali yake mbaya sana siku za nyuma lakini sasa hivi ukitoka juu kwenye ndege unaona Dodoma ilivyo ya kijani.
“Kigoma hoteli zimeshaanza kuvamiawa na maji na wataalam wametuambia maji yameongezeka mita 2,leo hii ukiendaa baadhi ya nchi utaona mazingira yalivyoharibika kutokana na uchafuzi wa mazingira,”amesema Jafo.
“Hii ni siku maalumu kwa ajili ya upandaji wa miti,nawashukuru waliokubali wito wa kukubali kuja katika siku hii ya upandaji miti.
“Nakushukuru wewe muandaaji wa hii shughuli naona umeratibu vizuri haya matembezi hata wale wenye vitambi leo wametembea na ninaimani kutembea leo cholesterol zimepungua,”amesema Jafo.
Pamoja na hayo, Waziri Jafo ameiagiza kila halmashauri nchini kupanda miti milioni moja na laki tano ambapo amesema wameanzisha kampeni ya mazingira ili kila mtu aweze kuhusika.
Amesema, kutakuwa na kampeni ya mazingira na hii ni kutokana na miti milioni 48 kila mwaka inakatwa hivyo kampeni hiyo itashirikisha kila mtu na hii itakuja na mashindano ambayo itashindanisha mikoa bora,halamashauri za wilaya,miji,kata na vijiji,vyuo, shule za msingi na sekondari na huku zawadi kama magari zikitolewa kwa washindi.
“Tunataka Tanzania iwe ya mfano na kwenye taasisi za Serikali tutapanda miti ya matunda,wakuu wa mikoa sasa tuhakikishe tunaenda kupanda miti katika maeneo yetu natamani kila mwanafunzi awe na miti mitatu na kuitunza jambo hili litakuwa jema sana na suala hili lishuke hadi kwenye ngazi za familia,”amesema.
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria