April 30, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kulia ni sehemu ya gereza la Mdellin, alilvyoikarabati Pablo Escobar baada ya kujisalimisha na kukubali kutumikia kifungo miaka 5

KWA TAARIFA YAKO: Huyu ndio tajiri wa dawa za kulevya dunia nzima

Alimililiki ndege zaidi ya 140, alilipa deni la nchi yake, aliua zaidi ya watu 4000

Na Mwandishi Wetu

Pablo akiwa katika moja ya ghala lake la fedha

Pablo Emilio Escobar Gaviria (PABLO Escobar) akiwa Bilionea wakati ana miaka 22, ndiye mtu pekee aliwahi kusafirisha dawa za kulevya nchini Marekani zaidi ya mtu yeyote ambapo aliingiza asilimia 80 ya dawa aina ya cocaine.

Mwishoni wa miaka ya 1980, Pablo alijitolea kulipa deni la nchi ya Colombia ambapo alilipa zaidi ya dola za Marekani bilioni 10 ili tu asihukumiwe kwa makosa mbalimbali. Wakati huo mtandao wake wa kusambaza dawa za kulevya, ulikuwa unaingiza zaidi ya dola za Marekani milioni 570 kwa wiki.

Kwa mujibu wa Roberto Escobar(ndugu wa Pablo), mtandao huo ulikuwa unatumia dola 2,500 kwa mwezi kununua raba bendi ili tu kufungia pesa zake.

Inadaiwa kuwa Pablo alihusika na vifo vya watu wasiopungua 4,000, ikijumuisha majaji 200 na polisi 1,000. Inadaiwa pia aliua waandishi wa habari na maofisa wa serikali. Aliwahi kulipua ndege mwaka 1989, ambayo iliua watu 110.

Pablo Escobar aliamua kujisalimisha mwenyewe na kukubali kutumikia kifungo cha miaka mitano mwaka 1991. Akiwa katika jela ya Medellin, nchini Colombia alikarabati eneo alilokuwa akikaa ndani ya gereza na kulifanya kuwa la kifahari na kisha kuweka watu wake ili kuendesha gereza hilo ambapo aliendelea na biashara yake ya dawa za kulevya.

Chumba cha kifahari alichokuwa analala kiongozi, mmiliki na tajiri wa mtandao wa dawa za kulevya, Pablo Escobar baada ya ukarabati katika jela ya Medellin, Colombia kilivyokuwa mwaka 1992. Picha ya AP

Inakisiwa kuwa panya walikula kiasi cha fedha zisizopungua dola bilioni 2 kila mwaka ambazo hutokana na faida kwani alikuwa akihifadhi fedha zake katika maghala (wherehouses) na maeneo yasiyo rasmi na kudai kuwa maeneo hayo ndio yalikuwa salama zaidi, japokuwa amekuwa akipoteza asilimia 10 ya mapato yake kwa kuliwa na panya kwa mwaka.

Kwa jinsi alivyokuwa na fedha nyingi, Pablo Escobar aliwahi kufanya hela kuwa kuni (kuwasha moto kwa kutumia dola milioni 2 za Marekani ) kwa madai kwamba mwanae anasikia baridi. Hivyo kutumia moto huo kumpa joto.

Mwishoni mwa miaka 1980, serikali ya Columbia ilikamata sehemu ya mali za Escobar ambapo zilikuwa ni ndege 142, helikopta 20, boti za kifahari 32, nyumba na maofisi 141.

Pamoja na kwamba alikuwa ndio mtu anayetafuta kuliko wote nchini Marekani wakati huo, Pablo akiwa na mwanae nje ya geti la Ikulu ya Whitehouse, na bado hawakumtambua na kumkamata.

Japo alikuwa ndio mtu anayetafutwa zaidi kwa uharamia wa dawa za kulevya nchini Marekani, Pablo na mwanae wa kiume waliwahi kupiga picha mbele ya lango la Ikulu ya Whitehouse (makazi ya rais wa Marekani) mwaka 1981 bila ya kutambulika.

Hadi mwaka 1993 utajiri wake ulikuwa unafikia dola za Kimarekani bilioni 30 ambapo kwa makadirio ya hadi sasa ni zaidi ya dola bilioni 53.5 (2020) zilizotokana na biashara hiyo haramu.

Pablo Escobar alifariki tarehe 2, disemba mwaka 1993 akiwa na umri wa miaka 44, akiwa katika mji wa Medellin, Antioquia, nchini Colombia. Chanzo cha kifo chake kikiwa ni majeraha ya risasi alizopigwa kichwani.