November 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akizindua tovuti ya E-fahamu iliyoanzishwa na Vodacom Foundation

Vodacom Foundation yazindua tovuti ya elimu E-fahamu

Na Joyce Kasiki,timesmajira online,Dodoma

KAMPUNI ya Vodacom Foundation imezindua tovuti  ya elimu iitwayo E-

fahamu yenye lengo la kuwasaidia walimu na wanafunzi kupata vitabu vya

ziada na kiada kwa shue za msingi na sekondari  ambayo inafuata mitaala

ya kutoka maktaba ya Taasisi ya Elimu Tanzania na masomo ya kimataifa

bure kwa njia ya mtandao.

Lengo la Tovuti hiyo  ni kuunga mkono juhudi za Serikali za kutoa

elimu bila malipo kwa shule za msingi na sekondari nchini.

Akizungumza wakati akizindua tovuti hiyo katika mashindano ya Sayansi

,Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) 2021 Waziri wa Elimu,Sayansi na

Tekonolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema,kwa kupitia tovuti hiyo

wanafunzi watajifunza  masomo  mbalimbali wanapotumia simu za

mkononi.

“Mtandao huu utaboresha elimu kwani italeta hamasa kwa wanafunzi

kujisomea kutokana na wanafunzi wengi kupenda kutumia simu za mkononi

.”amesema Profesa Ndalichako

Aidha Profesa Ndalichako amefurahishwa na kampuni hiyo

ilivyoshirikiana na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote kutoa Kompyuta na

Routers kwa wanafunzi .

Waziri Ndalichako ameiomba kampuni hiyo kuongeza vitabu zaidi katika

tovuti hiyo ili iweze kuwasaidia wanafunzi  kujifunza huku akitoa rai

kwa kampuni nyingine kuiga mfano wa Vodacom Tanzania Foundation

kutumia teknolojia kusaidia jamii.

Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Vodacom Foundation,Rosalynn Mworia

amesema  E- fahamu ni tovuti ya masuala ya kielimu inayopatikana

mtandaoni bure kwa ajili ya wateja wa Vodacom huku akisema kampuni

hiyo imeamua kutoa huduma hiyo bure kama sehemu ya kuunga mkono juhudi

za Serikali za kutoa elimu bila malipo kwa shule msingi na sekondari

nchini.                               

Amesema tovuti hiyo  ina nyenzo na taarifa muhimu  za kielimu kwa

ajili ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ikijumuisha masomo

ya Hisabati,Sayansi,Sanaa na Sayansi ya Jamii.

“Ili  kupata E- fahamu kwenye simu ama Kompyuta  utahitaji kuunganishwa

na huduma ya mtandao wa internet ya Vodacom au kutumia WiFI ambapo

baada ya hapo mhusika ataweza kuangalia video  za mafunzo ambapo

amesema  maudhui yanapatikana katika lugha za Kiswahili na Kiingereza

ambapo yapo katika muundo wa sauti,video,machapisho ya PDF na mazoezi

shirikishi.”amesema Mworia

Mworia amesema tovuti hiyo imeanza mwaka 2017 na tayari wamewafikia

jumla ya wanafunzi wapatao 150,000.