November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Afya ya Aubameyang yazidi kuimarika

ENGLAND, London

NAHODHA wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang amesema, familia yake ina wasiwasi na yeye kupungua uzito ghafla baada ya kuugua malaria mnamo Machi, na kwamba hali yake inazidi kuimarika polepole.

Aubameyang, mwenye umri wa miaka 31 raia wa Gabon, aliwekwa kando katika michezo minne baada ya kupata malaria alipokuwa kwenye jukumu la kimataifa na alikaa hospitalini mwezi uliopita kabla ya kurejea katika ushindi wa timu hiyo ya goli 2-1 dhidi ya Villarreal katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Ligi ya Uropa.

“Nilikuwa najisikia kawaida tu, nilidhani kwamba hiyo ilikuwa safari. Nilihisi nimechoka, haswa dhidi ya Liverpool, lakini nilifikiri ni kwa sababu ya safari. nilikuwa na siku tatu mfululizo, homa, mchana kutwa na usiku. Baada ya hapo, nilimfahamisha daktari. Baada ya hapo, aliingia hospitalini, ambapo alitibiwa kwa siku tatu na kupoteza 4kg.

“Ilikuwa wakati mbaya na familia yangu, ilikuwa na hofu kidogo kuniona hivi. Nina bahati nimepata matibabu kwa wakati unaofaa; usipotibu haraka inaweza kusababisha shida kubwa,” amesema Aubameyang.

Hata hivyo, Aubameyang alifunga bao katika mchezo wake wa kwanza tangu alipopona maradhi katika ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Newcastle United kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.

%%%%%%%%%%%%%%