Na Joyce kasiki, timesmajira,online,Dodoma
MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Charles Mbuge amewataka vijana waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya Jeshi hilo kwa kujitolea kwa mwaka 2020/21,kuripoti makambini kuanzia Mei 7 hadi 14 mwaka huu.
Vijana hao ni wale ambao waliochaguliwa na kuripoti makambini mwezi February mwaka huu walirejeshwa majumbani.
Akitoa taarifa hiyo juzi,Makao Makuu ya JKT jijini hapa kupitia waandishi wa habari,Kaimu Mkuu wa Utawala wa JKT Kanali Hassan Mabena amesema vijana wanaotakiwa kuripoti makambi ya JKT waliyokuwa wamepangiwa hapo awali ni wale wenye elimu ya Darasa la saba na kidato cha nne .
Kanali Mabena amefafanua kuwa vijana wenye elimu ya kidato cha sita ,ngazi ya cheti,stashahada ,shahada na wale wenye taaluma ya uhandisi wataendelea kusubiri majumbani hadi hapo utaratibu mwingine utakapotangazwa.
More Stories
Rais Samia aungwe mkono ajenda ya nishati safi ya kupikia
Ushiriki wa Samia G20 wainufaisha Tanzania
Dkt.Tulia ashiriki ibada, asisitiza waumini kushiriki uchaguzi serikali za mitaa