Na David John timesmajira online
KAMPUNI ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania imesema kuwa imeongeza igo wa upatikanaji wa huduma zake katika Mikoa ya Tanga Segerea ,Bukoba ,Morogoro kihonda,Mbeya,na Dodoma, lengo ikiwa ni kufikia mikoa na wilaya zote Tanzania .
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam Meneja Mauzo wa rejareja wa Kampuni hiyo Vennesy Chilambo amesema Puma energy imejipanga kikamilifu kwa kuwapa wateja wake huduma iliyobora.
Amesema licha ya mikoa hiyo lakini,mkoa wa Dar es Salaam wamebadilisha vituo vyao vya rejareja katika maeneo ya Oysterbay ,Upanga,Bagamoyo,na Ocean Road nakuwa katika muonekano mpya kabisa unaoleta uhalisia wa Kampuni hiyo.
“Hatua hii inalingana na ahadi ya kampuni yenye dhamira yake ya ” kuimarisha Jamii ” ili kukuza ukuaji na ustawi .tunaamini kabisa hitaji la kusaidia jamii Kwa kufanya upatikanaji wa Mafuta ya vilainishi vya bei rahisi Kwa ubora unaofaa na kiwango sahihi hapa nchini .”amesema Venessy
Akizungumzia kuhusu Kampuni hiyo ya Mafuta ya Puma Energy Venessy amesema ilisajiliwa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na inamilikiwa Kwa pamoja na Serikali ( kupitia Msajili wa Hazina ,Wizara ya Fedha ) .
Ameongeza kuwa pamoja na Puma investments kila moja ikiwa na umiliki wa hisa Kwa asilimia 50,kampuni ya hiyo ni ya mkondo wa kati kimataifa katika masuala ya Mafuta na inajihusisha na uhifadhi mkubwa na usambazaji.
More Stories
Gavu aanika miradi iliyotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita Geita
RC Makongoro: Samia aungwe mkono nishati safi ya kupikia
TAKUKURU,rafiki yanufaisha wananchi Mwanza