November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali yaja na mpango madhubuti wa kutokomeza malaria nchini

Na Mwandishi Wetu,TimesaMajira online, Arusha

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya inatarajia kuzidua utekelezaji wa afua ya kupambana na ugonjwa wa malaria nchini kwa kuanzisha upimaji wa malaria kwa wananchi katika kaya baada ya mmoja wao kugundulika ana maambukizi ya ugonjwa huo katika kituo cha afya.

Haya yamesemwa na Dkt.Samwel Lazaro naibu meneja mpango wa kuthibiti malaria wakati akifunga mkutano wa waandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani ambayo kitaifa yanatarajiwa kufanyika mkoani Arusha ambapo amesema kuwa Afua hiyo itazinduliwa na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee ma wWtoto Dkt.Doroth Ngwajima.

Dkt.Samwel amesema kuwa mikoa itayoanza na utekelezaji wa afua hiyo kwa awamu ya kwanza ni Arusha, kilimanjaro na Manyara ambapo mwakani wataongeza mkoa wa Njombe na mwaka 2023 wataongeza mkoa mwingine wa Iringa.

“Afua hii mpya inalenga kuhakikisha mikoa hii mitano inafikia kiwango cha maambukizi ya malaria kwa asilimia 0 ifikapo mwaka 2025 ambapo katika utelelezaji wake itakuwa ni kupima watu katika kaya ambapo kitakachofanyika ni mgonjwa atakapogundulika ana malaria atakapoenda kupima katika kituo cha kutolea huduma basi kutakuwa na ufuatiliaji katika ngazi ya kaya kwa wanakaya wote kupimwa ili kutibu na kuzuia kuendelea kusambaa kwa ugonjwa huo,” ameeleza Dkt.Samwel.

“Pia ikigundulika kuwa kunamazalia au chanzo cha mbu katika jamii hiyo kutakuwa na afua nyingine ya kuhakikisha hayo mazalia aidha ni madimwi yatapigwa dawa ili kuua mazalia hayo na mwisho wa siku ile jamii tutakuwa tumeikinga na maambukizi ya malaria,” amefafanua.

Aidha ameiomba jamii kushiriki kikamilifu kuhakikisha wanautokomeza ugonjwa wa malaria katika mikoa hiyo ifikapo mwaka 2025 ambapo mpango huo unawataka kupunguza malaria kufikia chini ya asilimia 3.5 kama nchi kwenye mikoa 5 ambayo iko chini katika maambukizi ya ugonjwa huo itahusika katika utokomezaji wa malaria kwa miaka mitano.

Kwa upande wake Mkuu wa ufuatiliaji na tathimini kitengo cha malaria Dkt. Sejenunu Aron amesema kuwa wanataka wafikie malengo ya Tanzania kutokuwa na malaria kabisa ambapo hadi sasa wameweza kupunguza wingi wa watu wanaopata malaria kwa asilimia 50 kutoka asilimia 14.8 ya mwaka 2015.

“Sambamba na hayo idadi ya vifo vitokanavyo na malaria imepungua kwa asilimia 61 huku mikoa ya Kigoma,Geita , Kagera,Mtwara na Ruvuma ikiea na kiwango cha juu ya asilimia 9 ya maambukizi ya Malaria,”amesema Dkt Sijenunu.

Amefafa nua kuwa Kigoma maambukizi yapo kwa asilimia 24.4, Geita 17.3, Kagera 15.4, Mtwara 14.8 na Ruvuma 11.8, huku mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Mbeya na Songwe wakiwa chini ya asilimia 1.