November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

BASATA yatoa onyo kali kuhusu mienendo ya wasanii

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

BARAZA la Saraa la Taifa (BASATA), limesikitishwa sana na Matukio na Mienendo ya Wasani hapa nchini katika mitandano ya kijamii kwa kushamiri vitendo vya matumizi ya Lugha zisizo na staha, Malumbano, Kukashfiana na hata usambazaji wa taarifa za Video zenye mwelekeo wa kudhalilishana.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Baraza la Sanaa imesema, Vitendo hivyo ni kinyume na Kanuni ya 25 (1) – (8) ya Kanuni za Baraza (Tangazo Ia Serikal Na. 43 ya mwaka 2018). Hivyo Baraza linatoa ‘Onyo’ na kukemea vikali mienendo na vitendo hivi na kuwataka wote wanaohusika kuacha mara moja tabia hiyo.

“Baraza litachukua hatua kali kwa Msanii yeyote atakaebainika kuendelea na kutenda vitendo ambavyo ni kinyume the Sheria na Kanuni zinazosimamia sekta ya Sanaa. Vitendo hivi vnarudisha nyuma juhudi za Serikali ya awamu ya sita (6) yenye nia ya dhati ya kuleta maendeleo na kukuza uchumi wa Wasanii, Wadau wa Sanaa na pato la Taifa kwa ujumla.

“Baraza linaamini na kusisitiza kuwa Sekta ya Sanaa hususani tasnia ya filamu na Mziki wa Tanzania tulipo sasa zinahitajika juhudi za Wasanii wenyewe kwa kujituma zaidi na kuongeza ubunifu ili kufikia tuzo kubwa za Kimataia kuliko kudhani uvumi wa ‘Kick’ zenye kuchafua, ndio njia ya kupata mafanikio katika Sanaa,” imesema taarifa ya Basata.

Aidha Baraza linategemea kuona hali ya upendo, Amani, Mshikamano na Ushnikiano miongoni mwa Wasani na Wadau wa Sanaa vinaendelezwa kama hapo awali .

%%%%%%%%%%%%%