November 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani Jokate Mwegelo akizugumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jana .

Mamlaka zatakiwa kushughulikia watu Matapeli nchini.

Na David John,Timesmajira Online,Kisarawe

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani Jokate Mwegelo amezitaka Mamlaka zinazoshughulikia Makosa ya uhalifu kwa njia ya mitandao kuharakisha uchunguzi kwani matapeli wameendelea kutumia jina lake kufanya utapeli kwa wananchi wanyonge.

Pia amewataka wananchi kuwa makini juu ya uhalifu unaondelea kwenye mitandao ambapo baadhi ya  watu wanatumia jina lake kufanya utapeli.

Jokate ameyasema haya jana wilayani hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisni kwake,amesema watu ambao nimatapeli  wanatumia jina lake kuwatapeli watu Kwa kile walichodai yeye anatoa mikopo jambo ambalo sio la kweli.

“Binafsi sina huduma yeyote ambayo naitoa juu ya utoaji wa mikopo kwa wananchi hivyo natoa tamko kwamba mimi sifanyi biashara wala huduma yeyote ya mikopo na sitarajiii kufanya Kwa sasa.”amesema Jokate

Nakuongeza “Mtu akituma nyaraka kwako jaribu kuwa makini na kuangalia hata hivyo wao kama wakuu wa wilaya hawana website na pia wanaonyesha hadifomu ya kugushi ya TRA na kuna Nyaraka nyingine inaonyesha inatoka Bungeni hivyo lazima wajiulize kabla ya kufanya jambo lolote. “amesema Jokate

Amesema kuwa  kipindi hiki watu  ni wajanja  hivyo jamii lazima iwe makini kwani teknolojia iko juu tofauti na wanavyofikiria na kwa yeyote anayetumia jina lake  kwamba anatoa mikopo ni waongo na ni matapeli hao.

“Watu Sasa hivi wanatumia majina ya viongozi nikiwemo mimi kwa manufaa yao hivyo lazima muwe makini na hapa niseme tu  kwamba 2015 ilitungwa Sheria ya uhalifu wa makosa ya  mtandaoni kwasababu ya mambo kama hayo  hivyo nivema kikashughulikia kikamilifu malalamiko hayo kwani watu wanazidi kutapeliwa.

“Naomba Mamlaka husika kuharakisha uchunguzi kwani watu wanaofanya mambo haya wanajulikana na  wanatumia namba za simu kimsingi watu wengi wanakutana na kadhia hii hivyo Mamlaka ziingie kazini watu wanaumia Sana.”amesema Jokate

Ameongeza kuwa elimu ya matumizi ya Tehama bado haijaingia vizuri kwa wananchi hivyo Mamlaka ni vema ifanye kazi zaidi kwani watu wengi wanatapeliwa sana na anaomba watu hao wakipatikana wahakikishe fedha zinarudi Kwa wahusika na Mamlaka zisipo fanya kazi yake wananchi wataendelea kulia.