Na Joyce Kasiki,TimesMajira Online,Dodoma
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Kakurwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier ambapo Balozi huyo ameeleza kufurahishwa na maendeleo makubwa yanayoendelea kufanyika pamoja na kusisitiza kuendeleza ushirikiano .
Mazungumzo hayo yamefanyika jana Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma amesema nchi yao imeahidi kugharamikia mafunzo ya ufundi kwa vijana Kwa asilimia 100.
Amesema nchi yao imefikia uamuzi huo baada ya kufurahiswa na mipango ya Serikali ya awamu ya tano chini Rais Dkt.John Magufuli ya kuwezesha vijana.
“Nchi kwa sasa ina muelekeo mzuri baada ya kufikia hatua ya uchumi wa kati, hivyo ni habari njema kwa watanzania na ni muelekeo mzuri katika mashirikiano ya uwekezaji, na tumevutiwa sana na Hotuba aliyoitoa Mhe. Rais Magufuli jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa bunge la 11 kuhusu mikakati ya ukuzaji wa sekta binafsi nchini,”amesema na kuongeza
“Baada ya Uchaguzi Mkuu miaka hii mitano ijayo ni miaka ya kufanya kazi, ushindi wa CCM umekuwa mkubwa sana licha ya changamoto ndogo ndogo zilizojitokeza lakini Uchaguzi umekwisha salama na serikali imeshaundwa na sasa ni muda wa kuchapa kazi na mikakati ya maendeleo ni mizuri na nina imani ushirikiano wetu utaimarika zaidi,” amesema Balozi Clavier
Aidha, Katibu Mkuu ameeleza kuwa, mazungumzo hayo yamelenga kuimarisha ushirikiano katika ujenzi wa vyuo vya ufundi ili kukuza upatikanaji wa ajira, na pia kuimarisha zaidi sauti ya Tanzania Katika Jumuiya za Kimataifa, kwa kuzingatia kuwa sauti ya Tanzania kihistoria imekuwa kubwa na hasa katika maeneo ya Usalama, Amani na katika Mfumo wa Umoja wa Mataifa kuchangia Amani Afrika na nje ya Afrika, na CCM itaendelea kuilekeza seriakali kuongeza juhudi katika ushirikiano huo.
Huu ni utaratibu wa Viongozi wa Chama kuendelea kujenga na kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na mataifa mengine yenye nia njema ya Nchi yetu.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â