Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
KINARA wa mabao wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) John Bocco amechaguliwa kuwa
Mchezaji Bora wa mwezi Novemba msimu wa 2020/21, huku nafasi ya Kocha Bora ikichukuliwa na Charles Boniface Mkwasa anayeinoa timu ya Ruvu Shooting.
Mshambuliaji huyo na Nahodha wa klabu ya Simba, ametwaa tuzo baada ya kuwashinda mshambuliaji wa Ruvu Shooting, Abdulrahman Mussa na mshambuliaji wa Young Africans SC, Deus Kaseke alioingia nao fainali.
Sasa Bocco anaungana na wachezaji wengine ambao ni Prince Dube wa Azam (Septemba) na Mukoko Tonombe wa Yanga (Oktoba) katika orodha ya nyota ambao tayari wameshatwaa tuzo
hiyo.
Kwa upande wa Mkwasa aliwashinda Mecky Maxime wa Kagera Sugar FC na Fulgence Novatus wa Gwambina FC baada ya kuiongoza Ruvu Shooting kutoka nafasi ya 10 hadi ya nne katika msimamo wa Ligi ikishinda michezo mitatu dhidi ya Coastal Union, Mbeya City na Tanzania Prisons huku wakipata sare mbili dhidi ya Mwadui na Kagera Sugar.
Makocha waliotwaa tuzo hiyo ni Aristica Cioaba aliyekuwa Azam FC (Septemba) na Cedric Kaze wa Yanga (Oktoba).
More Stories
Samia awazawadi Stars milioni 700/-
Samia atoa bilioni 8/- kukarabati viwanja vya CHAN, AFCON
Rasmi Chatsoko mdhamini mkuu wa Goba Hills Marathon 2025