October 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

ZEC yatangaza wajumbe Viti Maalumu Wanawake Baraza la Uwakilishi

Na Jaala Makame Haji – ZEC

TUME ya Uchaguzi ya Zanzibar ZEC imetangaza wajumbe 18 kutoka Chama Cha Mapinduzi kwa nafasi ya Viti Maalum vya Wanawake vya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC ), Jaji Mkuu Mstaaf, Hamid Mahmoud

Tume imetangaza majina ya Wajumbe hao katika mkutano wake uliofanyika tarehe 07/11/2020 katika ukumbi wa mikutano wa Tume hiyo Maisara mjini Zanzibar.

Tangazo hilo limetolewa baada ya kuridhika kuwa wote wanasifa ya kuwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kama zilivyoainisha katika Katiba ya Zanzibar ibara ya 68.

Waliotangazwa na Tume ya Uchaguzi ni pamoja na Panya Ali Abdallah, Bihindi Hamad Hassan, Salma Mussa Bilali, Shadya Moh’d Suleiman, Fatma Ramadhan Mohamed (Mandoba), Sada Ramadhan Mwenda na Mwantatu Mbaraka Khamis.

Wengine ni Zainab Abdalla Salum, Riziki Pemba Juma, Leila Muhamed Mussa, Salha Mwinyi Juma, Hudhaima Mbarak Tahir, Sabiha Fil fil Thani, Aza Januar Joseph, Mwanaid Kassim Mussa, Mgeni Hassan Juma, Mwanajuma Kassim Makame na Rahma Kassim Ali.

Tume tayari imeshawasilisha Majina ya Wajumbe hao kwa Katibu wa Baraza la Wawakilishi kwa ajili ya Hatua nyengine za Kisheria.