Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza
MECHI ya Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) iliyochezwa juzi kwenye uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza kati ya wenyeji KMC dhidi ya Yanga imeingiza zaidi ya Shilingi milioni 57.7.
Katika mchezo huo KMC walikubali kichapo cha goli 2-1 ambapo walitakungulia kupata goli dakika ya 27 lililofungwa na Hassan Kabunda huku lile la Yanga la kusawazisha likifungwa dakika ya 41 na Tuisila Kisinda lakini mshambuliaji Waziri Junior akiifungia Yanga goli la ushindi dakika ya 61.
Mapato hayo ni mara mbili zaidi ya yale yaliyopatikana mara ya mwisho Yanga kucheza katika uwanja huo kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Alliance ambao waliingiza Sh. milioni 28.
Meneja wa uwanja huo, Jonathan Mkumba amesema, baada ya kufanya mahesabu walikuwa wamekusha milioni 57.7 ambazi zitaganywa kwa Serikali ambao wanachukua asilimia 18 (VAT) na wao kama wamiliki wa uwanja wanchukua asilimia 15.
Baada ya KMC kupelekea mechi yao kwenye uwanja huo, pia wanaziomba timu nyingine ikiwemo Gwambina kuchezi mechi zao kwenye uwanja huo ili kuwapa burudani wakazi wa jiji hilo lakini pia kujiongezea kipato kupitia mechi zao.
“Timu nyingi zinategemea viingilio vya mechi zao kujiendesha, hivyo tunaziomba timu mbalimbali ikiwemo Gwambina kutumia uwanja huu kwani watakapokutana na timu kama Simba na Yanga mapato yao yanaweza kuzidi haya tuliyoyakusanya sasa,” amesema Meneja huyo.
Hata hivyo kiongozi huyo pia amewaomba Yanga kuona kama wanaweza kupeleka mechi zao katika uwanja huo kwani kama watu walijitokeza na kuwapa sapoti kubwa katika mechi zao za msimu uliopita ambapo kikosi chao kilikuwa na changamoto, msimu huu wanaweza kupata mashabiki wengi zaidi kutokana na kuimarika kwao.
“Msimu huu kikosi cha Yanga kimeonekana kuimarika zaidi hivyo tunaamini kuwa endapo wataamishia huku baadhi ya mechi zao basi watapata mashabiki wengi zaidi hata ya ilivyokuwa mwaka jana ambapo walitumia uwanja huu kwa ajili ya mechi zao za kimataifa, “amesema Mkumba.
More Stories
Samia awazawadi Stars milioni 700/-
Samia atoa bilioni 8/- kukarabati viwanja vya CHAN, AFCON
Rasmi Chatsoko mdhamini mkuu wa Goba Hills Marathon 2025