Na.Mwandishi.Wetu,TimesMajira
BENKI ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imechaguliwa kuwa miongoni mwa washindi wa Tuzo za Ubora wa Uandaaji na Uwasilishaji wa Taarifa za Fedha kwa mwaka 2025 (Best Presented Financial Statements Awards), zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).
Hafla ya utoaji wa tuzo hizo imefanyika leo, tarehe 26 Novemba 2026, kuanzia saa 12:00 jioni katika ukumbi wa APC, Bunju, Dar es Salaam.

Mafanikio haya ni ushahidi wa dhamira endelevu ya Benki katika kuzingatia viwango vya kimataifa vya uandaaji wa taarifa za fedha, kuimarisha uwazi, uwajibikaji na utawala bora, pamoja na kuzingatia matakwa ya kisheria na kiudhibiti.
Tuzo hii inaendelea kuimarisha hadhi ya TADB kama taasisi ya fedha ya maendeleo inayozingatia weledi na ubora katika utekelezaji wa majukumu yake.


More Stories
Mwanasheria Mkuu azindua mifumo ya kidijitali kuelekea dira 2050
Waziri Homera aipongeza TANESCO kwa mafanikio kutimiza miaka 95
Makosa ya kibinadamu chanzo MV Mwanza kugonga mwamba