November 25, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwanasheria Mkuu wa Serikali arejesha tabasamu kwa Wananchi Arusha

Na.Mwandishi wetu,TimesMajira

MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amemuhudumia mwananchi aliyekuja kupata huduma ya ushauri wa kisheria wakati wa uzinduzi wa Kliniki ya Sheria bila malipo kwa wananchi wa mkoa wa Arusha tarehe 24 Novemba, 2026

Johari amemsikiliza na kumuhudumia Euralia Matai ambaye aliwasilisha changamoto ya ardhi inayomkabili.

Aidha, Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikabidhi suala hilo kwa jopo la Mawakili wa Serikali wanaotoa huduma kwenye Kliniki hiyo na kuahidi kulitatua kwa haraka na kumrejeshea haki yake Matai.

“Tumeyapokea malalamiko yako na mimi pamoja na timu tutayafanyia kazi kwa haraka ili kuweza kutatua changamoto inayokukabili”.Amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Timu ya Mawakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imepiga kambi katika Uwnaja Sanawari Jijini Dar es Salaam kutoa huduma mbalimbali za kisheria bila malipo kwa wananchi wa mkoa wa Arusha kuanzia tarehe 23 hadi 29 Novemba, 2026.