
Na Israel Mwaisaka, Rukwa
SHULE 10 za msingi wilayani Nkasi zimepongezwa na kupewa zawadi ya kilo 25 ya sukari kwa Kila shule kwa kufanya vizuri katika mtihani wa taifa wa darasa la Saba 2026 huku nyingine 10 zikipongezwa kwa kupandisha ufaulu.
Akikabidhi zawadi hizo k kwenye hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri makamo Mwenyekiti wa halmashauri Joseph Mwenda amessema halmashauri imefanya hivyo kuwatia moyo Walimu kutokana na matokeo mazuri yaliyopelekea Wilaya Nkasi kushika nafasi ya kwanza kimkoa na 19 kitaifa.
Alisema kuwa kushika nafasi ya kwanza kimkoa siyo jambo dogo na kuwa hilo kwao limewapa faraja kubwa na kuwataka waendelee kujituma katika mazingira haya haya yaliyopo na kuendelea kushika nafasi hiyo ya kwanza.

Akitoa taarifa ya matokeo ya darasa la Saba mwaka huu Kaimu mkurugenzi mtendaji wa Wilaya Eliud Njogela alidai kuwa Wilaya Nkasi imeongoza kimkoa kwa kupata 85.2%,Manispaa ya Sumbawanga imeshika nafasi ya pili kwa kupata 81%, Wilaya ya Kalambo imeshika nafasi ya tatu kwa kupata 76% na Wilaya ya Sumbawanga imeshika nafasi ya 4 kwa kupata 75%.

Alisema kuwa pia shule 10 zimeweza kupandisha ufaulu katika shule zao na kuwa Imani Yao ni kuona mwakani shule hizo zinaingia kwenye ushindani mkubwa utakaoiwezesha Wilaya Nkasi kuendelea kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa na ndiyo maana nazo zimepewa motisha ya kilo 25 kwa Kila shule.
Mbunge wa jimbo la Nkasi kasikazini Bazilio Kapunda Mbwilo kwa upande wake alisema kushika nafasi ya kwanza ni hatua moja lakini kazi iliyopo mbele yao ni kuilinda nafasi hiyo na kuwataka waongeze bidii na kuwa wao kama viongozi wapo tayari Kutoa msaada wowote ule pale utakapohitajika kwa lengo la shule hizo ziendelee kufanya vizuri.
Alisema kuwa anajua Walimu wengi wanapitia changamoto mbalimbali na kuwa zisiwakatishe tamaa bali ziwatie nguvu katika kutekeleza majukumu Yao wakati wao kama Wabunge wakiendelea kuieleza Serikali juu ya changamoto wanazozipitia na kuwa Kuna siku changamoto hizo zitapungua kwa kiasi kikubwa.
Shule 10 zilizoingia kumi bora ni Azakita,Kisura,Matala,Nkata,Mvimwa, Namanyere,Ntatumbila, Muungano na shule ya msingi Malongwe.
Shule zilizopandisha ufaulu ni shule ya msingi Nkata kwa alama 60,Kalila 56,Kate 49,Mandakelenge 44,Lyapinda 33,Nkundi 32,Tambaruka 29,Chobga 24,Kanchui 21 na Sintali imepandisha alama 11.

Walimu kwa upande wao wameeleza changamoto wanazozipitia na kuomba Serikali kuendelea kushughulika nazo ili waweze kufanya kazi hiyo katika mazingira mazuri yatakayowawezesha wao kufanya vizuri zaidi na kuendelea kuilinda nafasi yao ya kwanza kimkoa na lengo lao ni kushika nafasi ya kwanza kitaifa.

More Stories
Azania kutoa mikopo ya riba nafuu kwa wanawake
Uongezaji thamani Madini kupewa kipaumbele TMIC 2026
TTCL yatambuliwa kimataifa kwa huduma za ftth