November 4, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanaodaiwa kupanga kufanya fujo hukumu ya Lisu waonywa

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online,Dar

JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar-es-Salaam limetoa onyo kwa kundi la watu wanaodaiwa kuhamasisha ndani na nje ya Mkoa huo kufanya fujo siku ya Novemba 6 mwaka huu wakati wa hukumu ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Tundu Lisu katika Mahakama Kuu Tanzania .

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar-es-Salaam Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Jumanne Murilo amesema, kuna taarifa mbalimbali kuwepo kwa kundi la watu wenye lengo la kufanya fujo,na vurugu au hujuma siku hiyo.

“Jeshi la Polisi linatoa onyo kali kwa kundi la watu ,waliopanga kuja Dar-es-Salaam kuhamasisha vurugu siku ya Ijumaa wakati wa hukumu ya Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lisu.Jeshi la Polisi litazuia na kushughulika na mtu yoyote au kikundi kitakachobainika kuwa katika mipango hiyo ya fujo,”amesema Murilo .

Amesema vurugu au hujuma ya aina yoyote Jeshi la Polisi Kanda Maalum halitavumilia viashiria vyovyote,vya uvunjifu wa amani na litachukua hatua za haraka na za kisheria.

Pia amesema,jeshi hilo linawataka wananchi kuheshimu utaratibu uliowekwa na Mahakama jinsi ya kufatilia mashauri mbalimbali.