Na.Mwandishi Wetu,TimesMajira
WIZARA ya Maliasili na Utalii, chini ya uongozi wa Waziri Dkt. Ashatu Kijaji, imeeleza utayari wake wa kuimarisha ushirikiano na taasisi ya Six Rivers Africa, inayofadhiliwa na Sir. Jim Ratcliffe, mmoja wa wamiliki wa klabu ya Manchester United, katika kukuza uwekezaji kwenye sekta za uhifadhi na utalii nchini Tanzania.
Hayo yameelezwa jana , mjini Manchester, Uingereza, wakati wa kikao kati ya Waziri Dkt. Kijaji akiwa ameambatana na timu yake, akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi, na Mwenyekiti wa Bodi ya Six Rivers Africa,Glenn Turner.

Katika mazungumzo hayo,Turner ameeleza dhamira ya taasisi hiyo kwa kushirikiana na Sir Jim Ratcliffe kuongeza uwekezaji nchini Tanzania katika sekta za uhifadhi na utalii, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kulinda rasilimali za asili na kukuza utalii.




More Stories
Serikali yaendelea kupunguza makali ya bei za mafuta
Serikali yafungua milango ya uwekezaji Sekta ya Nishati
Wanaodaiwa kupanga kufanya fujo hukumu ya Lisu waonywa