October 29, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kawaida atoa ufafanuzi majukumu ya Chipukizi,Vijana CCM

Na Mwandishi Wetu,Timesmajira

MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM)Mohammed Ali Kawaida (MCC) amejibu na kutolea ufafanuzi kuhusu kuwepo wa Chipukizi wa CCM na Vijana wa Itifaki na Hamasa wa UVCCM.

Kawaida akizungumza leo Oktoba 28, 2026 akiwa Jimbo la Chamwino, Dodoma amesema kuna kiongozi wa Vijana wa Chama pinzani ambaye alipotosha umma kuhusu matumizi ya makundi hayo mawili na yeye ameamua kutolea ukweli wa majukumu yao.

“Kazi ya Chipukizi sio kufanya siasa, sio kupewa agenda za siasa, kazi ya Chipukizi ni kuwalea ndio maana kauli mbiu yao inasema elimu na malezi,” amesema Kawaida

Pia kuhusu Vijana wa Itifaki na Hamasa ambao wanaofahamika kikanuni, Kawaida ametolewa ufafanuzi akisema;

“Ndani ya UVCCM hatuna kikundi cha usalama, hatuna makomandoo wala maaskari ila ndani ya UVCCM tunao vijana wa Itifaki na Hamasa ambapo hata mimi (Kawaida) nimetokea,”