
Na Israel Mwaisaka, Nkasi
Kaimu Katibu tawala wa mkoa Rukwa Donald Nsoko amewataka viongozi mahala pa kazi kutambua michango ya Watumishi wao kwa kuwapatia motisha mbalimbali zitakapelekea kuwapa hari ya kufanya kazi kwa bidii na weledi.
Ameyasema hayo Leo katika kikao kazi alichofanya na Watumishi wa Serikali wilayani Nkasi katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya kilicholenga kupokea kero mbalimbali za Watumishi na kuzitafutia ufumbuzi.
Amesema kuwa mahala popote pa kazi ambapo michango ya Watumishi imekuwa ikitambuliwa na kuthaminiwa hata matokeo yake huwa makubwa na kuweza Kutoa huduma stahiki kwa jamii wanayoihudumia.
Kaimu Katibu tawala huyo alifafanua kuwa mahala popote ambapo viongozi wamekua wakitambua michango ya Watumishi wao wadogo matokeo ya kiutendaji uonekana na kuleta tija.
Pia aliwakumbusha Watumishi wa umma kuzingatia wajibu na ndipo haki ifuate kwa maana haki na wajibu vinakwenda sambamba na kuwa kwa kufanya hivyo Kila upande utakua umetendewa haki.

Sambamba na hilo alidai kuwa migogoro makazini inaweza kutatuliwa kwa njia za wazi huku akisisitiza umuhimu wa utatuzi wa migogoro kwa haraka pale inapojitokeza ili kuleta utengamano na kazi ziweze kufanyika kwa tija.
Na katika kikao hicho Watumishi wa umma walikumbushwa kufuata kanuni za kiutumishi na kujua mipaka Yao ya kazi kama kanuni ya ajira zao zinavyoelekeza na kuwa hilo litaondoa migongano kati Yao.
Suala la kufuata sheria na kanuni za kiutumishi pia lilipewa kipaumbele ambapo ilielezwa kuwa mtumishi yeyote anayefuata kanuni na Sheria zote za kiutumishi wakati wa utekezaji wa majukumu yake ni ngumu sana kwa Mtu wa namna hiyo kupata matatizo kazini.

Kikao hicho kilienda sambamba na kupokea kero za Watumishi ambapo nyingi zilitafutiwa ufumbuzi wa papo hapo na nyingine kubebwa kwa ajiri ya utatuzi zaidi.

More Stories
Ndejembi awataka vijana kutokuwa watazamaji Sekta ya Gesi na Mafuta
Serikali yaimarisha utafutaji wa Mafuta,Gesi
SGA Cash in Transit yatajwa kuwa kampuni bora ya huduma