October 12, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Dkt,Samia mgeni rasmi kilele cha mbio za Mwenge kitaifa Rukwa

Na Israel Mwaisaka, Rukwa 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa Mgeni rasmi katika maadhimisho ya  kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026 mkoani Rukwa.

Maadhimisho hayo yatafanyika  Oktoba 14, 2026 katika Uwanja wa Nelson Mandela uliopo katika Mji wa Sumbawanga mkoani Rukwa.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi ofisi ya Rais na maendeleo ya vijana Joel Nanauka akizungumza katika kikao na wanahabari kilichofanyika mjini Sumbawanga leo ambacho pia kilihudhuriwa na Waziri wa vijana,ajira na uwekezaji Zanzibar Ali Suleiman Ameir .

Alifafanua kuwa maadhimisho ya kilele hicho yanaenda  sambamba na kuzimwa rasmi kwa Mwenge wa Uhuru Kitaifa ambao uliwashwa Zanzibar Aprili 04 mwaka huu na  Rais na Mwenyekiti wa Mapinduzi ya Nzanzibar Ali Hassan Mwinyi ambapo umekimbizwa katika Halmashauri 195 zilizopo katika mikoa 31 Bara na Visiwani.

Aliongeza kuwa kuelekea maadhimisho hayo Waziri wa Elimu Prof. Adolf Mkenda kwa niaba ya Waziri Mwigulu Nchemba alifungua wiki ya Vijana Kitaifa Oktoba 10 mwaka huu ambayo ilianza rasmi Oktoba 08 katika Uwanja wa Ndua mjini hapa na itahitimishwa 0ktoba 14.

Aidha maadhimisho ya kilele cha Mwenge wa Uhuru Kitaifa kitaendana na ibada takatifu ya kumbukizi ya miaka 27 ya kifo cha baba wa Taifa mwalimu Julias Kambarage Nyerere itakayo fanyika katika kanisa Katoliki la mtakatifu Epifani saa 12:00 asubuhi mjini Sumbawanga.

Aidha Nanauka amewaalika wananchi kujitokeza kwa wingi kushuhudia maadhimisho hayo.