KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni, na Michezo ikiongozwa na Mwenyekiti Mhe. Husna Sekiboko (Mb) imepokea na kuchambua taarifa ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhusu Maandalizi ya Mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON 2027) .
Kamati imepokea taarifa hiyo, Agosti 17, 2026 katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma ambayo imewasilishwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Hamisi Mwinjuma.
Mhe. Mwinjuma aliwasilisha pia Maendeleo ya ujenzi na ukarabati wa viwanja vitakavyotumika, pamoja na taarifa ya Kanzidata ya ajira katika sekta ya Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo.
Baada ya uwasilishaji, Wajumbe wa Kamati hiyo waliuliza maswali na kutoa maoni na maswali ambayo Mhe. Mwinjuma aliyafafanua kwa kina.

More Stories
UDOM yaweka mkazo Ubunifu kukabili changamoto za Taifa
Elimu, Utafiti, Ujuzi, Ubunifu kujenga Tanzania imara
Dkt.Lingwanda apongeza ubunifu wa vijana katika maonesho ya NACTVET