
Na Israel Mwaisaka, Rukwa
Serikali kupitia Wizara ya Madini imethibitisha uwepo wa madini ya dhahabu katika Kijiji cha Nchenje, Wilaya ya Nkasi, Mkoani Rukwa.
Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Peter Lijualikali, amesema baada ya kupata viashiria vya uwepo wa madini katika eneo hilo, Serikali iliwatafuta wataalamu kwa ajili ya kufanya utafiti.
Amesema utafiti huo umebaini uwepo wa madini ya dhahabu, chuma na shaba, huku dhahabu ikiwa na kiwango cha asilimia 70 katika eneo hilo.
Kwa upande wake, Kamishna wa Madini Mkoani Rukwa, Mhandisi Joseph Kumbulu, amesema uchimbaji wa madini hayo unatarajiwa kuanza mwezi Septemba mwaka 2026.
Mhandisi Kumbulu amesema hadi sasa wachimbaji 12 wamekwisha kata leseni za uchimbaji, huku Serikali ikiendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu uwepo wa madini hayo pamoja na fursa za kiuchumi zinazotokana na shughuli za uchimbaji.

More Stories
EMS yapanua wigo utoaji huduma kidigitali
Maji salama ya wafikia wakazi 22,482
Masenza Mwenyekiti JUWAKITA MwanzaÂ