Na Mwandishi wetu,Timesmajiraonline,Idodi.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge Uratibu na Wenye Ulemavu) Prof, Palamagamba Kabudi amesema Serikali itaendelea kuheshimu na kuthamini mchango wa kiuongozi uliotolewa na aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera Bunge Uratibu na Wenye Ulemavu) Marehemu William Lukuvi.
Hayo ameyasema Agosti 15,2026 wakati wa maadhimisho ya ibada ya Misa Takatifu ya kumaliza Msiba iliyofanyika nyumbani kwa Marehemu Idodi Mkoani Iringa na kuhudhuriwa na wananchi na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali.

Amesema , “Enzi za uhai wake Waziri Lukuvi alinisaidia kufahamu shughuli mbalimbali za Bunge na serikali na hivyo kupata weledi mzuri mambo mengi kutokana na uzoefu aliyokuwa nao,”
Aidha uwezo wake wa kusimamia nidhamu ipasavyo Bungeni ikiwa ni pamoja na kuimarisha mahusiano kati ya Serikali na Bunge ilimfanya aendelee kuaminiwa katika kazi ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu.

Kwa Upande Mama Germana Lukuvi Mjane wa Marehemu ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kushikamana na familia tangu walipopata msiba.
Awali Mbunge wa Isimani Emanuela Mtatifikolo alisema Marehemu Lukuvi ataendelea kuishi kwenye mioyo ya wananchi wa Isimani, kwa mageuzi makubwa ya maendeleo aliyoyafanya.

“Uwakilishi wake kwa wananchi wa Jimbo la isimani na kwa kushirikiana na Serikali aliwezesha Jimbo la Isimani kunufaika na ujenzi wa barabara ya lami uimarishaji wa Huduma za afya na kuendelea kuboresha miundo mbinu ya elimu sambamba na umeme,” alibainisha


More Stories
Kituo cha Saratani kuwa kimbilio kwa wananchi Mbeya
Mkenda:Ujuzi agenda kuchochea ajira kwa vijana
Zimebaki siku sita uzinduzi wa JNHPP