August 13, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Gereza kwamngumi lamkabidhi aliyekuwa mfungwa vifaa vya ujenzi



Na Mwandishi wetu


GEREZA la Kwamngumi mkoani Tanga limemkabidhi aliyekuwa mfungwa, Ndugu Tumaini Mahuji, vifaa mbalimbali vya ujenzi baada ya kumaliza kutumikia kifungo chake katika gereza hilo.


Zoezi hilo lilifanyika Agosti 11, 2026, likiongozwa na Mkuu wa Gereza la Kwamngumi, Mrakibu wa Magereza (SP) Francis Makelemo.


SP Makelemo amesema Jeshi la Magereza linaendelea kutoa fursa kwa wafungwa kupata elimu, ujuzi na maarifa ya ufundi stadi, pamoja na vitendea kazi vinavyowawezesha kujitegemea baada ya kurejea katika jamii.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Bw. Ally Mkwavinga, amesema juhudi hizo ni muhimu katika kuwaandaa wafungwa kurejea katika jamii wakiwa na uwezo wa kujitegemea.


Kwa upande wake, Ndugu Tumaini Mahuji ametoa shukrani kwa serikali na Jeshi la Magereza kwa kumkabidhi cheti cha VETA pamoja na vifaa vya ujenzi vitakavyomwezesha kutumia ujuzi alioupata kujipatia kipato na kusaidia familia yake.


Vifaa alivyokabidhiwa ni pamoja na pima maji, msumeno wa mbao, nyundo, tape measure, kobilo, koleo na sululu.