Na Mwandishi wetu,Timesmajira
MWENYEKITI wa taasisi ya Ongea na Mwanao, Steve Nyerere, kesho atawaongoza watanzania kwenye dua maalumu ya kuwaombea wasanii, wachezaji na Waandishi wa habari waliotangulia mbele ya haki.
Steve amebainisha kwamba shughuli hiyo ya dua kwa wasanii waliotangulia mbele ya haki itaanza saa tatu asubuhi, itaongozwa na masheikh na wachungaji
Hayo amebainisha leo, Julai 31, 2026 jijini Dar es Salaam na kuwaomba watanzania kushiriki kwenye tukio hilo linalojenga umoja kwa nchi na Taifa Kwa ujumla.
“Kesho tutawakumbuka makundi yote, ya wasanii, wachezaji, Waandishi wa Habari, viongozi mbalimbali waliotangulia mbele ya haki,” amesema.
Pia kuelekea shughuli hiyo amewaasa vijana kwa makundi yote kulinda amani ya Taifa kwa unyenyekevu na heshima kubwa Kwa maslahi ya nchi.

Nyoshi El Saadat, naye amesema kuwa amesema jambo hili ni kubwa na la kupongeza na kuomba watanzania wote kujitokeza katika dua hiyo.
Abdallah Mkumbila, “Muhogo Mchungu”, amesema kuwa jambo la kuwaombea dua waliotangulia mbele ya haki ni jambo jema kwa maana Kwa maelezo ni kwamba pale kaburini hatujui palivyo,” amesema.
Ally Choki, kesho ni siku ya baraka kuwaombea ndugu zetu waliotangulia mbele ya haki, naomba wote watnzania wajitokeze.
Andrew Sekidia, waliotangulia wametuachia amani ambayo inafanya hadi leo tuendelee kufanya majukumu yetu vema , hivyo tuendelee kudumisha amani.
Salum Abdul ‘Chiky’ ambaye ni mwenyekiti wa chama Cha Waigizaji Tanzania, amesema kesho wanakutana kwa ajili ya kuwaombea wenzatu, tunaamini hata malaika watakuwepo nawaombeni mfike kwa wingi.

More Stories
Onyo kali latolewa dhidi ya Utoroshaji wa Dhahabu Kahama
Bayport Yaadhimisha Miaka 20 kwa Kutoa Vifaa vya TEHAMA Kibamba
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ashiriki uzinduzi wa boti mpya za doria