July 22, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kituo cha afya Ibungilo chafikia asilimia 25

Na Judith Ferdinand, Timesmajira Online- Mwanza 

SERIKALI kupitia Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza,imeendelea na jitihada za kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya karibu kwa kuanza ujenzi wa kituo cha afya Ibungilo ambao umefikia asilimia 25 ya utekekalezaji.

Ujenzi wa kituo cha afya Ibungilo kilichopo Kata ya Ibungilo,unatekelezwa kwa kutumia fedha za mapato ya ndani ya Halmshauri  ya Manispaa ya Ilemela kwa thamani ya zaidi  ya sh.bilioni 1.3 pamoja na ongezeko la thamani ya kodi (VAT).

Ambao  unatekelezwa na kampuni ya M/s SUMA JKT Construction Company Limited ambapo hadi kukamilika kwake unatarajiwa kuwa na jumla ya ghorofa tatu.

Mhandisi wa Halmashauri  ya Manispaa ya Ilemela Mussa Maroba,ambapo amesema awamu ya kwanza ya ujenzi umefikia asilimia 25 ukijumuisha ujenzi wa msingi,nguzo mlalo,nguzo wima,ujenzi wa “lift”katika ghorofa zote tatu,kupaua na kuezeka na unatarajiwa kukamilika Desemba 2026.

 Ambapo ujenzi wa kituo hicho utakapokamilika unatarajiwa kunufaisha takribani wananchi 190,575 kutoka Kata 7 ikiwemo Ibungilo,Nyamanoro,Nyasaka, Kawekamo,Pasiansi na  Ilemela.

“Kituo hiki kitapunguza umbali wa upatikanaji wa huduma za afya wa kutembea km 4,utapunguza msongamano wa wagonjwa katika kituo cha afya Buzuruga na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sekou-Toure pamoja na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa upatikanaji wa huduma za upasuaji wa dharura,”amesema Mhandisi Maroba.

Hata hivyo ikumbukwe  kuwa fedha za mapato ya ndani zinatokana na kodi ya huduma yaani  “service levy” ambayo hutumika kutekeleza miradi ya maendeleo.