Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Maafisa wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wanaendelea kuwahudumia wananchi wanaotembelea Banda la TTCL katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026), kwa kuwapatia elimu kuhusu huduma na suluhisho mbalimbali za mawasiliano na teknolojia za kidijitali zinazotolewa na TTCL.
Katika banda hilo, wananchi wanapata fursa ya kujionea huduma za intaneti ya kasi ya juu, suluhisho za kidijitali kwa matumizi ya nyumbani na biashara, pamoja na kupata ushauri wa kitaalamu kuhusu bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na TTCL.
Sambamba na hilo, TTCL inaendelea kuwapatia wateja ofa maalum za Sabasaba, zikiwemo vifaa vya mawasiliano vinavyopatikana kwa bei zenye punguzo kubwa, pamoja na huduma mbalimbali zinazolenga kurahisisha maisha na shughuli za kila siku katika mazingira ya kidijitali.
Akizungumza katika maonesho hayo, Meneja wa Banda, Janeth Maeda amesema ushiriki wa Shirika katika Sabasaba 2026 unalenga kuwasogezea wananchi huduma, kuongeza uelewa kuhusu bidhaa na huduma zinazotolewa na TTCL, pamoja na kujenga mahusiano imara na wateja na wadau mbalimbali.
Aidha, alibainisha kuwa maonesho hayo yanatoa fursa kwa Shirika kupokea mrejesho wa wateja ili kuendelea kuboresha huduma na kuendana na mahitaji ya soko la mawasiliano linalobadilika kwa kasi.
Aidha,wananchi na wadau wanaotembelea banda hilo wanapata fursa ya kutumia buree public Wi-Fi inayopatikana katika viwanja hivyo ili kufahamu speed ya intanet ya TTCL.
TTCL inaendelea kuwakaribisha wananchi wote kutembelea Banda la Shirika hilo katika Viwanja vya Mwalimu Julius K. Nyerere ili kujionea teknolojia bunifu, kupata elimu kuhusu huduma za mawasiliano na kunufaika na ofa maalum zinazopatikana katika kipindi chote cha maonesho.

More Stories
ACT Wazalendo yapinga zuio la mikutano ya hadhara
Prof. Rasheli apongeza shughuli za REA Sabasaba 2026
Wizara yasuluhisha mgogoro wa Kampuni na Mkandarasi