
J
Na Mwandishi Wetu.
UONGOZI wa JKT Tanzania, ukiongozwa na baadhi ya viongozi wake pamoja na mchezaji Hassan Wahabi, umemtembelea kiungo wa Yanga SC, Pacôme Zouzoua, anayepatiwa matibabu baada ya kuumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.
Pacôme alipata jeraha wakati wa mechi kati ya Yanga na JKT Tanzania iliyochezwa Juni 30, 2026 katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, na kulazimika kutolewa nje ya uwanja kwa matibabu.

Miongoni mwa waliofika kumjulia hali nyota huyo ni Afisa Habari wa JKT Tanzania, Masau Bwire, ambaye aliungana na ujumbe wa klabu hiyo kutoa pole na kumtakia nafuu ya haraka.
Hatua hiyo imepongezwa na wadau wa soka kama ishara ya mshikamano na utu ndani ya mchezo, huku wakimtakia Pacôme apone haraka na kurejea uwanjani kuendelea na majukumu yake.

More Stories
Dereva wa John Heche afariki Kigoma, damu zatapakaa
TTCL yajipanga kuwahudumia wateja Sabasaba 2026
VETA yatumia Sabasaba kuonesha ujuzi na ubunifu wa Vijana