Na Mwandishi Wetu,Timesmajira
Mjasiriamali na Mwanzilishi wa Pedima Enterprises Limited, Peter Didas Mallya (PEDIMA), ameendelea kuipeperusha bendera ya Tanzania kimataifa baada ya kutwaa tuzo mbalimbali zinazotambua mchango wake katika ubunifu, teknolojia na ujumuishaji wa huduma za kifedha.
Mwaka 2026, Peter Didas Mallya alitangazwa mshindi wa tuzo ya Tech Startup of the Year katika East Africa Change Makers Awards 2026, tuzo inayotolewa kwa wabunifu na kampuni zinazochangia maendeleo ya Afrika Mashariki kupitia teknolojia na ubunifu.
Katika mwaka huohuo, Kampuni yake ya Pedima Enterprises Limited ilitwaa tuzo ya Financial Inclusion Company of the Year kwenye Africa Company of the Year Awards (ACOYA) 2026, kwa kutambua mchango wake katika kukuza ujumuishaji wa huduma za kifedha na matumizi ya teknolojia barani Afrika.

Ushindi huo unaongeza orodha ya mafanikio ambayo Peter Didas Mallya amekuwa akiyapata katika safari yake ya ujasiriamali na uongozi. Miongoni mwa tuzo alizowahi kushinda ni Founder of the Year Award (FOYA) 2023, Africa Company of the Year Awards (ACOYA) 2024 na 2025, CEO Top 100 Awards 2024 na 2025, pamoja na Global Recognition Award 2025.
Kupitia Pedima Enterprises Limited, Mallya ameendelea kuongoza maendeleo ya suluhisho za kidijitali zinazolenga kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha, kuwawezesha mawakala wa huduma za fedha na kuharakisha matumizi ya teknolojia katika sekta ya fedha nchini Tanzania.
Akizungumzia mafanikio hayo, Peter Didas Mallya amesema kila tuzo aliyopokea ni uthibitisho kwamba ubunifu, uadilifu na kujituma vinaweza kuleta mabadiliko makubwa katika jamii.
“Mafanikio haya ni ya timu nzima ya Pedima, washirika wetu na wateja wetu ambao wameendelea kutuamini. Tutaendelea kubuni suluhisho zinazorahisisha maisha ya Watanzania na kuchangia maendeleo ya sekta ya teknolojia na huduma za kifedha barani Afrika,” amesema.
Kwa miaka kadhaa sasa Peter Didas Mallya ameendelea kutambulika kama mmoja wa wajasiriamali wanaochochea ukuaji wa sekta ya teknolojia ya kifedha (fintech) nchini Tanzania kupitia mifumo na huduma zinazochangia ujumuishaji wa kifedha, matumizi ya teknolojia na ukuaji wa uchumi wa kidijitali.

More Stories
Ndejembi: Bomba la mafuta EACOP lafikia hatua za mwisho
Wakulima Mil. 1.3 kunufaika na teknolojia ya kidigitali
Kamati ya Bunge yaridhishwa na Mradi wa JNHPP